Mbunge wa Kigoma Kaskazini(CHADEMA)Mh,Zitto Kabwe
---
Zitto Kabwe:'Ujumbe amenitumia Daktari yupo pale MOI‘Kaka Zitto,hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad,I agree with you this is outright outrageous’.
Nimechukizwa sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya
kwa Dr Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea
kuyasikia kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala
badala ya kutumia njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia
wanaoamini ni maadui zao katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi
za usalama kuteka raia, kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.
Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi
ya madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba
majeruhi huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa
jana usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika
msitu wa MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado
hazijathibitishwa na vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.Kusoma Zaidi Tamko la Zitto Kabwe Bofya na Endelea......>>>>>>
No comments:
Post a Comment