Afisa
Mtendaji Mkuu wa benki ya CBA, Bw Yohane Kaduma akimkabithi mfano wa
hundi yenye thamani ya Tsh Millioni 5 kwa makamu wa pili wa Raisi wa
Zanzibar Balozi Seif Idd, Afisa Mtendaji Mkuu wa CBA Bw Kaduma amesema
benki yake iko tayari kuikopesha serikali ili iweze kununua meli mpya
ili kuhakikisha inaboresha huduma za usafiri majini.Nae balozi Seif Idd
ameshukuru msaada huo kutoka CBA na ametoa wito kwa wadau mbalimbali na
serikali kuitembelea benki hiyo ili kuona ni jinsi gani taifa linaweza
kufaidika hasa kwenye kuisaidi serikali kuboresha usafiri majini
Na Mohammed Mhina, Zanzibar
Wakati Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa kwenye mchakato wa kutafuta fedha za
kununua meli mpya, Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), imesema iko tayari
kuikopesha SMZ fedha za kununulia Meli hiyo.
Afisa Mtendaji
Mkuu wa Benki hiyo Bw. Yohane Kaduma, amesema benki yake iko tayari
kuipitia SMZ mkopo wa kununulia Meli hiyo endapo watakubaliana na
kushirikishwa kwenye mchakato huo.
Bw. Kaduma alikuwa
akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Zannzibar mara baada ya
kukabidhi msaada wa shilingi milioni 5, kwa Makamu wa pili wa Rais wa
Zanzibat Balozi Seif Ali Iddi ili kusaiidia ghala za matibabu kwa
majeruhi na ubani kwa wafiwa wa ajali ya Meli ya Skagit.
Bw. Kaduma amesema
kuwa endapo Benk yake itaombwa kutoa mkopo huo inaweza kufanya hivyo
ili mradi tu kukaa meza moja na Serikali na kukubaliana aina ya mkopo
pamoja na mambo mengine.
Awali akipokea
msaada huo, Makam wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, amesema kuwa
pamoja na kusimamishwa kwa baadhi ya meli za watu binafsi kuchukua
abiria, SMZ pia imeagiza meli zake kufanyiwa uchunguzi kama zinafaa
kuchukua abiria.
Balozi Seif
amesema kuwa ameziagiza Mamlaka ya usafiri majini Zanzibar na Sumatra,
kuzifanyia uchunguzi meli hizo za SMZ ikiwemo MV Maendeleo ambayo
imerejea siku za karibuni ikitokea Mombasa nchini Kenya ambako ilikuwa
katika matengenezo makubwa.
Amesema Serikali
haiwezi kukaa kimya huku ikiona kuwa wananchi wake wanapatwa na majanga
ya mara kwa mara kutokana na kusafiri kwa meli zisizo na uhakika.
Katika hatua
nyingine idadi ya maiti za MV Skagit, imeongezaka hadi kufikia 128 baada
ya maiti nyinine mbili kupatikana leo karibu na Kisiwa cha Chumbe nje
kidogo ya mji wa Zanzibar na nyingine sita zikipatikana mkoani Tanga.
Tofauti na taarifa
za awali kuwa maiti tano zilipatikana Bagamoyo mkoani Pwani, ifahamike
kuwa maiti hizo zilipatikana katika fukwe za bahari wilayani Pangani na
nyingine mjini Tanga.
Kwa mujibu wa
Taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoani Tanga ACP Costantine Masawe, maiti
nne ikiwemo ya mwanamke mmoja zilipatikana huko Pangani na nyingine
mbili ikiwemo ya mwanamke mmoja zikapatikana kwenye fukwe za bahari
mjini Tanga.
Kamanda Masawe
amesema kuwa maiti zote zilichukuliwa vipimo kwa ajili ya uchunguzi wa
Vinasaba (DNA) pamoja na kupigwa picha kabla ya kuzikwa.
Hata hivyo Kamanda
huyo wa Polisi amesema kuwa maiti moja kati ya hizo, ilitambuliwa kuwa
ni ya Mohammed Saidi Salum mkazi wa Ziwani Chakechake mkoa wa Kusini
Pemba ambaye alitambuliwa baada ya simu aliyopatikana nayo kufanyiwa
uchunguzi.
Hadi
sasa maiti ambazo hazijapatikana ni 16 kutokana na kupatikana kwa watu
146 wakiwa hai ikilinganishwa na idadi ya watu 290 waliokuwemo ndani ya
meli hiyo ya Skagit siku ya tukio.
No comments:
Post a Comment