Balozi wa
Heshima wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon katika jiji la mapesa la New York
City (NYC) nchini Marekani ambaye pia ni mcheza sinema na mlimbwende maarufu
kutoka jiji hilo linaloaminiwa kuwa kitovu cha pesa duniani, Mmarekani Deidre
Lorenz ameahidi kukisadia kituo cha watoto yatima cha Upendo kilichopo katika
Manispaa ya Moshi.
Lorenz
alikitembelea kituo hicho siku mbili (tarehe 22 Juni) kabla ya kukimbia mbio za
Mt. Kilimanjaro Marathon zilizotimua vumbi tarehe 24 juni mwaka huu kuanzia
Moshi Club hadi Rau mudukani.
Mbio za
Mt. Kilimanjaro Marathoni zilianzishwa na Marie Frances anayetoka katika jiji
la matajiri la Bethesda nje kidogo ya jiji la Washingyon DC nchini Marekani
mwaka 1991 baada ya kuombwa na balozi wa zamani nchini Misri.
Marie
Frances aliyekuwa muandaaji wa vipindi vya television ya ABC alianzisha mbio za
Pyramid Marathon zilizofana sana nchini Misri na kumfanya balozi wa Tanzania
nchini Misri wakati ule kumuomba aje Tanzania kuanzisha mbio za marathon.
Mt.
Kilimanjaro Marathon ilianzishwa mwaka 1991 katika Manispaa ya Moshi zikiwa ni
mbio kukimbia kwa furaha (fun run) inayowaleta wazungu kupanda mlima
Kilimanjaro, kukimbia na kwenda kutembelea mbuga zetu za wanyama. Mbio hizi
zipo katika kiundi la Seven Continental Marathons ambazo hukimbiwa katika
mabara saba ya dunia.
Deidre
Lorenz ambaye amewahi kuigiza katika filamu nyingi alipatikana katika bahati
nasibu (Raffle) iliyochezeshwa na Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 wakati wa mbio
za New York Marathon jijini New York Marekani mwaka 2011. Katika bahati nasibu
hiyo Deidre Lorenz aliibuka mshindi na kujipatia tiketi ya bure pamoja na
gharama za hoteli za kuja kukimbia mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon mwaka huu.
Wadhamini
wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon ni kampuni ya ndege ya Ethiopia Airlines
(ET) ambayo huwa inantoa tiketi za bei rahisi kwa wale wanaokuja kukimbia mbio
hizo. ET pia hugharamia ushiriki wa Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 katika mbio
za New York Marathon, Boston Marathon na Los Angelos Marathon ili kijitangaza.
No comments:
Post a Comment