Monday, July 9, 2012

EPIQ BONGO STAR SERCH YAENDELEA KUSAKA VIPAJI ARUSHA, JANA 25 WALIPATA BAHATI YA KURUDIA AWAMU YA PILI LEO KUSIKILIZWA TENA.



Majaji wanapo Choka kazi inakua ngumu kwelikweli lakini ndio kazi hapa kila mmoja hajitambui watu ni wengi wanaojitokeza mkoani humo.
Mmoja wa washiriki akionyesha uwezo wake wa kupiga gitaa mbele ya majaji.
Foleni ni kubwa lakini vijana wanakomaa hadi hatua ya mwisho.
Madam Ritta akimpongeza mmoja wa washiriki wa shindano hilo.
Meneja wa Mauzo wa Zantel kanda ya Kaskazini Kimolo Melitus akichangia damu kutokana na zoezi hilo kuenda sambamba na uchangiaji damu.

KATIKA yaliyojiri siku ya kwanza ya usaili ni wingi wa washiriki waliojitokeza kuonyesha vipaji vyao ambapo iliwalazimu baadhi kuombwa kurudi tena siku ya Pili (leo) ili kuweza kupata nafasi ya kukuonana na majaji.
 
Ikiwezeshwa na Zantel kumekuwa na matokeo ya kijamii ambayo yamekuwa yakiendelea. Kubwa zaidi ni uchangiaji wa damu ambao umekuwa ukienda sambamba na usahili na muitikio wa washiriki pamoja na wafanyakazi wa Zantel katika kuchangia damu umewezesha zoezi zima kuwa la mafanikio.
 
Hadi sasa usailli wa kupata washiriki watano bora watakaouwakilisha mkoa wa Arusha unaendelea. Zaidi ya washiriki 25 wamepata nafasi ya kuwaona majaji kwa mara ya pili.
 

No comments:

Post a Comment