Monday, July 9, 2012

HALMASHAURI YA WILAYA MERU YAWAPA MAFUNZO YA KOMPYUTA MAAFISA WAKE



NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA

HALIMASHAURI ya wilaya ya Meru imefanikiwa kuwapeleka Maafisa utumishi
wa halimashuri hiyo kozi maalum ya kutumia mfumo wa kompyuta katika
ulipaji wa mishahara ili kuthibiti ubadhirifu wa mishahara hewa ambao
umekuwa ukitokea mara kwa mara  .

Hayo yalisemwa na mkurugenzi  mtendaji wa halmashauri  hiyo Trasias
Kagenzi alipokuwa akiongea  katika kikao cha baraza la madiwani  wa
halmashauri hiyo.

Aidha Kagenzi alisema kuwa kwa sasa halimashauri hiyo itakuwa inalipa
wafanyakazi wake mishahara bila kuwepo usumbufu kwa kuwa hapo awali
mahesabu yalikuwa yanasumbua hali iliyokuwa ikipelekea kutokea kwa
upotevu wa fedha nyingi.

“tumeona ni vema tukawapaeleka afisa utumishi kozi ambayo itawasaidia
kupata elimu  juu  ya kuthibiti fedha za halimashauri  kwa kutumia
mfumo wa kompyuta kwa kuwa fedha zilikuwa zinapotea mara kwa mara
“alisema

Alisema kuwa kupitia kozi waliyoipta maafisa hayo itwasaidia hata
katika kuthibiti swala zima la mishahara hewa amabyo imekuwa ikitolewa
kwa watu wasiojulikana hivyo kuifanya halmshauri kuingia hasara kubwa
.
Aliongeza kuwa  kwa sasa  mahesabu yote na ulipaji mishahara
yatafanyika kwa mpango maaluma ambao utakuwa ukizingatia mfumo huo
ambao hata wafanyakazi watakuwa na  unafuu wa kupata  mishahara yao
kwa wakati husika.

Kwa upande mwingine mkurugenzi huyo aliwataka madiwani wa halimashauri
hiyo kuhakikisha kuwa wanasiamamia kikamilifu miradi mbali mbali
iliyomo katika kata zao huku wakiweka nguvu katika kubuni vyanzo
vingine vya kuingiza mapato kwani bado wana upungufu wa fedha katika
miradi.

“sisi tunayo majukumu ya kubuni vyanzo vingine vya mapato kwani tuna
upungufu wa zaidi ya shilingi bilioni moja kwenye miradi yetu hali
inayopelekea baadhi ya miradi kukwama hivyo kushindwa kusonga
mbele”alisema Kagenzi

No comments:

Post a Comment