Friday, July 27, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA NA KUKAGUA CHUO KIKUU CHA NELSON MANDELA JIJINI ARUSHA LEO


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mwilongo na Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha Nelson Mandela ‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’, Prof. Burton Mwamila, kwa pamoja wakifurahia mtandao wa mawasiliano kwa njia ya Video unaowawezesha wanafunzi kuonana na kuzungumza na kuchangia masomo kutoka sehemu tofauti ndani na nje ya mkoa huo  wa Arusha, wakati Makamu alipofika chuoni hapo leo, kutembelea na kukagua chuo hicho kinachotarajia kuanza kusajili wanafunzi hivi karibuni. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo hicho.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozwa na Makamu wa Mwenyekiti wa Chuo kipya cha Nelson Mandela ‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’, Prof. Burton Mwamila, wakati leo akitembelea mazingira ya Chuo hicho kinachotarajia kuanza kusajili wanafunzi hivi karibuni kilichopo Jijini Arusha. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chuo cha Nelson Mandela ‘The Nelson Mandela African Instute Of Science and Technology’, Prof. Burton Mwamila, wakati akimfafanulia kuhusu kazi za maabala mpya inayoandaliwa katika Chuo hicho wakati Makamu alipofika chuoni hapo leo,  kutembelea na kukagua chuo hicho kinachotarajia kuanza kusajili wanafunzi hivi karibuni. Makamu wa Rais ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo hicho. Kushoto kwake ni mkewe Mama Asha Bilal.

No comments:

Post a Comment