Thursday, July 26, 2012

MAWAKALA WA KUANDAA MASHINDANO YA MISS UTALII WANATAKIWA




MISS UTALII TANZANIA WAJIIMARISHA KANDA YA KASKAZINI, WAKURUGENZI WA KANDA NA MIKOA WATEULIWA
Bodi ya taifa ya Miss tourism Tanzania Organisation , imefanya na kuthibitisha uteuzi wa wakurugenzi wa kanda na mikoa ya kanda ya Kaskazini, ambao pia  watakuwa na jukumu la kusimamia na kuandaa mashimdano ya Miss Utalii Tanzania , katika ngazi za mikoa ya Arusha,Manyara , Kilimanjaro na kanda ya Kaskazini. Bodi ilipokea zaidi ya maombi 12 kutoka kwa watu binafsi na makampuni mbalimbali, ambao waliomba ukurugenzi na uandaaji wa mashindano ya
Miss Utalii Arusha, Manyara na Kilimanjaro, ambopo waliofanikiwa kupitishwa na kuteuliwa ni Mr. Job lay Mr. Zephaniah Tumbo wa NAMAN 2010 LTD ( Arusha na Kanda ya Kaskazini) Mosses Method Komba wa NEW VISION PLAN COMPANY LTD (Manyara) na Kilimajaro). 

Bodi imezingatia vigezo vyote vya kanuni na taratibu za mashindano ya Miss Utalii Tanzania,katika kufanya uteuzi huo, ikiwemo kigezo cha kuwa na ofisi ya kudumu katika mkoa au kanda husika, kigezo kingine ni
waombaji kuwasulisha mpango mkakati wa kuimarisha na kukuza mashindano,Utalii na utamaduni katika mkoa au kanda husika kupitia mashindano haya. 

Bodi inaendelea na mchakato wa kupitia na kupokea maombi mapya na ya zamani ya kuandaa na kusimamia mashimdano ya Miss Utalii Tanzania , katika mikoa yote na kanda zote za Kusini, Kusini Nyanda za Juu,Mashariki, Kati, Zanzibar, Ziwa, Magharibi na kanda za Vyuo Vikuu. Mikoa ambayo maombi yanakaribishwa ni pamoja na mikoa ya RUVUMA, RUKWA, NJOMBE, KIGOMA, SHINYANGA, SHIMIYU, GEITA, TANGA, PWANI, SINGIDA, MTWARA, MWANZA, DODOMA, ZANZIBAR, MOROGORO NA TABORA. Kanda ambazo maombi yanakaribishwa ni pamoja na KANDA ZA KUSINI, KUSINI NYANDA ZA JUU, MASHARIKI, KATI, MAGHARIBI, ZIWA. Upande wa vyuo Vikuu maombi yanayo pokelewa ni ya kanda za MISS UTALII TANZANIA VYUO VIKUU KUSINI, KASKAZINI, MASHARIKI, MAGHARIBI, KATI, KUSINI NYANDA ZA JUU NA ZIWA


Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30-7-2012. Wakati huo huo kamati ya Taifa ya uratibu na ufundi ya mashindano ya Miss Utalii Tanzania , imetangaza kalenda mpya ya mashindano ya ngazi zote za Wilaya hadi taifa, kwa kuzingatia kalenda na utaratibu mpya wa fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania kila mwaka kuwa zinafanyika,9-12-2012 sambamba na sherehe za uhuru wa Tanzania kuanzia mwaka huu. 

Kalenda ya fainali za Wilaya na Mikoa yote sasa itakuwa imekamilisha mashindano ya ngazi zao hadi kufikia Oktoba 2012 na Kanda zote zutakuwa zimekamilisha fainali za kanda zote kufikia Novemba 12 ,2012.

Miss Tourism The Symbol Of National Heritage
Maombi yote yatumwe kupitia: missutaliitanzania@gmail.com

No comments:

Post a Comment