Thursday, July 26, 2012

MBABE WA APR YANGA USO KWA USO NA AZAM FC FAINALI KOMBE LA KAGAME BAADA YA KUICHAPA APR BAO 1-0


 Mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuz, akiwa amembeba mshambuliaji mwenzake, mfungaji pekee wa bao la ushindi la Yanga dhidi ya APR, Hamis Kiiza, wakishangilia baada ya mchezo huo wa hatua ya Nusu Fainali uliopigwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kumalizika.

Katika mchezo huo timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu huku timu hizo zikienda mapumziko zikiwa sare ya bila kufungana na hadi zilipomalizika dakika 90 za mchezo huo timu hizo zilishindwa kufungana na kuingia katika muda wa dakika za nyongeza.

Ilikuwa ni dakika ya 10 katika dakika 15 za kwanza za kati ya 30 za muda wa nyongeza, bao pekee a kichwa katika mchezo huo lililofungwa na Hamis Kiiza limeipa Yanga tiketi ya kucheza Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kwa mara ya pili mfululizo, ambapo sasa timu hiyo itakipiga na  Azam FC, siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kiiza alifunga bao hilo, baada ya krosi nzuri iliyopigwa na Haruna Niyonzima baada ya mpira wa kurushwa 'chap chap' wakati Said Bahanuz akiwazuga mabeki wa APR alipoanguka huku akiwalalamikia kumchezea vibaya huku Niyonzima akianziwa mpira huo wa kurusha na kumimina korosi iliyomkuta Kiiza na kuuzamisha mpira huo kimiani.

Dakika tatu baada ya bao hilo, beki wa Yanga, Godfrey Taita, alitolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na sasa ataukosa mchezo wa fainali kati yao na Azam siku ya Jumamosi.
Wachezaji wa Yanga, wakishangilia bao la Hamis Kiiza, lililodumu hadi mwisho wa dakika za nyongeza kumalizika na kuwapa raha wana Yanga.

No comments:

Post a Comment