Sunday, July 29, 2012

MBUNGE RITA KABATI AISAIDIA JEZI TIMU YA TASWA IRINGA



Mbunge Rita Kabati (kushoto) akimkabidhi mwenyekiti wa TASWA mkoa wa Iringa Bw.Francis Godwin seti ya jezi kwa ajili ya timu ya TASWA jana
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mhe. Rita Kabati (CCM) ameisaidia jezi seti moja timu ya waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) mkoa wa Iringa kama njia ya kuiunga mkono timu hiyo katika kuhamasisha michezo mkoani Iringa.

Akikabidhi msaada huo leo kwa mwenyekiti wa TASWA mkoa wa Iringa Bw.Francis Godwin ,mbunge Kabati alisema kuwa amelazimika kutoa msaada huo kama sehemu ya kuunga mkono unzishwaji wa timu hiyo .

Kwani alisema suala la michezo lime katika ilani ya uchaguzi wa CCM hivyo akiwa kama mbunge ameguswa na mkakati wa wanahabari mkoa wa Iringa katika kuhamasisha michezo na kuwa miongoni mwa wadau wa kweli wa michezo ambao wamekuwa wakiandika habari za michezo ila pia na wao wenyewe kuonyesha mfano katika michezo kwa kuwa na timu yao.

Mbunge Kabati alitoa wito kwa wabunge wengine na wadau wa michezo katika mkoa wa Iringa kujitokeza kuisaidia timu hiyo vifaa vya michezo pamoja na misaada mbali mbali pale inapohitajika ili kuiwezesha kuwa timu bora katika mkoa wa Iringa.

No comments:

Post a Comment