Miaka kumi tangu kupotea kwa bia iliyopata umaarufu na heshima kubwa miaka ya
2010 kurudi nyuma maarufu kama KIBO GOLD BIA, Kampuni ya bia ya
Serengeti iliyokuwa ikizalisha bia hiyo, imezindua tena bia hiyo na
kuingiza sokoni tayari kutumika kama vinywaji vingine vinavyozalishwa na
kampuni hiyo.
Akizungumza
na wageni waalikwa na waandishi wa habari waliohudhuria katika uzinduzi
huo uliofanyika katika kiwanda cha Serengeti tawi la moshi mkoani
Kilimanjaro, Meneja wa bia ya Serengeti bw. Alln Chonjo , amesema
kampuni hiyo merefu na kuamua kuizalisha tena ili kukidhi mahitaji ya
wateja wake na watanzania kwa ujumla.
“Leo
ni siku ya furaha kubwa kwetu Serengeti breweries kuona umati mkumbwa
wa watanzania mmehudhuria katika uzinduzi huu siku ya leo ambapo tuna
irudisha tena sokoni bia yetu ya KIBO GOLD ikiwa na muonekano uleule,
ladha ileile, na ubora uleule iyofanya bia hii kupata umaarufu mkubwa
ilipokuwa sokoni miaka michache iliyopita” alisema Chonjo na kuongeza
kuwa bia hiyo itauzwa kwa bei ya shs.1500 tu. Hali ambayo inaweza kuwa
faida kwa watanzania wote wenye mapenzi mema na kampuni ya bia ya
Serengeti.
Kwa
upande mmoja wa wakongwe katika utumiaji wa bia ya kibo gold wakati
inatengenezwa na na kampuni ya bia ya kibo breweries wakati ule kabla
haijafa,bw Julius Nyaki ameishukuru na kukipongeza kampuni ya bia ya
Serengeti kwa kurudisha bia hiyo sokoni ambapo sasa inarudi tena
ikiwazalishwa na kampuni ya bia ya Serengeti kiwanda cha Moshi makoani
Kilimanjaro na kuuzwa nchi nzima.
Sambamba na tukio hilo , kampuni ya bia ya Serengeti kupitia promotion inayoendelea maarufu kama
VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO imekabidhi zawadi ya pikipiki mpya kwa
mshindi wake bw. Vicent Lymo mkazi wa kibosh mkoani kilimanjaro
aliyejishindia zawadi hiyo kupitia promotion hiyo.
No comments:
Post a Comment