Meya
wa Manispaa ya Mosho Mjini, Jafari Michael(kushoto) akicheza kuashilia ufunguzi
rasmi wa mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa katika klabu ya
Makanyaga Mkoani Kilimanjaro mwishoni
Meya
wa Manispaa ya Mosho Mjini, Jafari Michael (kuli) akimkabidhi t-shirt na pesa
nahidha wa timu ya Makanyaga wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano ya Safari
Pool ngazi ya Mkoa wa Kilimanjaro
KAMPUNI ya
Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Safari Lager leo imekabidhi vifaa vya michezo katika mikoa
mitano inayoshiriki mashindano ya Safari Pool Taifa ambayo yanatarajiwa kuanza
leo katika mikoa hiyo
Vifaa
hivyo t-shirt pamoja,pesa za nauli kwa kila timu na pesa za zawadi kwa timu
zitakazoshinda katika fainali za mikoa hiyo ambazo wamekabidhiwa manahodha wa
kila klabu shiriki.
Mikoa
iliyokabidhiwa vifaa na pesa hizo ni Shinyanga,Kilimanjaro,Manyara,Tabora na
Kagera.
Makabidhiano
hayo yalifanywa na wageni rasmi mbalimbali kila Mkoa ambapo Tabora alikuwa
Ofisa utamaduni wa Wilaya, Mark Katunzi,Shinyanga alikuwa Ofisa Utamaduni wa
Wilaya, Asha Mbwana, Kagera alikuwa, Ibrahim Mabruk, Manyara alikuwa, Ofisa
Elimu ya Watu Wazima, Fausta Akoro na Kilimanjaro alikuwa Jafari Michael ambao
kwa ujumla waliwataka wachezaji wa Pool kuuheshimu mchezo na kuwa na nidhamu
katika kipindi chote cha mashindano na watambue kuwa kwenye mashindano lazima
apatikane mshindi wa kwenda kushiriki Taifa kuuwakilisha Mkoa.
Aidha
waliishukuru Kampuni ya Bia Tanzania kwa kufadhili mashindano hayo kwani
yanawafanya vijana faidike na kiasi cha fedha wanachoshindania licha ya
burudani waipatayo ambayo inawaepusha na mambo mengi yasiyo na faida mtaani
Mashindano
hayo yanatarajiwa kuanza kesho na
kumalizika Julai 8 mwaka huu ambapo timu itakayoibuka bingwa kwa upande wa Mkoa
itajinyakulia kitita cha sh. 700,000
huku mchezaji mmoja mmoja akiondoka na sh. 350,000 kwa upande wa wanaume na
wanawake wa kwanza atazawadiwa sh. 250,000 taslimu.
mshindi wa
pili kwa upande wa timu, atazawadiwa sh. 350,000, mshindi wa tatu, 200,000, wa
nne sh. 100,000 na kifuta machozi cha sh. 50,000 kitatolewa kwa timu zitakazoshiriki.
Halikadhalika
kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja kwa upande wa wanaume mshindi wa pili
atapata sh. 200,000, wa tatu sh. 150,000 na wa nne sh. 100,000 ambapo wanaume
kwa wanawake wanne kati ya wanane watakaopoteza mchezo katika awamu ya pili watazawadiwa
sh. 50,000, na wakataopoteza katika awamu ya kwanza wanane kati ya 16
wataambulia sh. 20,000.
Aidha kwa
upande wa wanawake kwa mchezaji mmoja mmoja mshindi wa pili atazawadiwa sh.
150,000, wa tatu sh. 100,000 na wa nne ataambulia sh. 50,000.
No comments:
Post a Comment