Afisa Maendeleo ya Biashara Mobile Ticketing Limited Bw.Albert Muchuruza
akiwaonesha waandishi wa habari njia muhimu za kukata tiketi za mabasi
kwa njia ya Mobile Ticketing kwa wasafiri wanaotumia mabasi yaendayo
mikoani,anaeshuhudia kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo Juma
Mgori.
KAMPUNI ya Mobile Ticketing Tanzania Limited imezidi kuboresha huduma
zake kufuatia kurahisisha zaidi upatikanaji wa tiketi za kusafiria
kwenye Selcom Pay Point kama zinavyopatikana huduma nyingine muhimu
nchini.
Uboreshaji huo umekuja kutokana na kampuni hiyo kutambua umuhimu mkubwa
wa huduma hiyo katika jamii ili kuzidi kuwarahisishia hata wale
wasiokuwa na simu za mikononi waweze kupata huduma hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini,Afisa Maendeleo ya Biashara
wa kampuni hiyo, Albert Muchuruza, alisema kuwa amefikia uamuzi wa kuwa
na huduma hiyo huku ikiendelea kushirikiana na Vodacom kwaajili ya
kuhakikisha huduma hiyo ya tiketi popote inamfikia kila mwananchi hapa
nchini.
"Tuko kwenye hatua za mwisho za kukamilisha vitu vichache japo huduma
hii ya upatikanaji wa tiketi za Usafiri wa Mabasi wa Mabasi kupitia
wakala wa Selcom Pay Point kama zinavyopatikana huduma nyingine za
kulipia ANKARA za maji, umeme, ving'amuzi nk, imeshaanza kutumika hapa
nchini lengo likiwa ni kuhakikisha huduma hii inapatikana kwa urahisi
zaidi na kumfikia kila mtu.
Aidha, Muchuruza alisisitiza kwamba huduma hiyo ya upatikanaji wa tiketi
kwenye selcom pay point imekwishaanza kufanya kazi siku chache
zilizopita na kuiomba jamii itambue mchango wa kampuni yake ambao ni
kurahisisha na kuweka huduma kama hiyo karibu na jamii kitu ambacho ni
uzalendo.
Mbali na hayo, pia Muchuruza alisifu muitikio chanya wa wananchi juu ya
utumiaji wa huduma hiyo ya tiketi popote na kusema kuwa tathmini
iliyofanywa na kampuni yake inaonyesha kuwa jamii imeanza kutambua na
kuelewa umuhimu na matumizi sahihi, hadi sasa muitikio ni mkubwa na
wenye kuridhisha kwa kipindi kifupi cha mwezi mmoja tangu huduma hiyo
kuzinduliwa mapema mwezi uliopita. |
No comments:
Post a Comment