Wednesday, July 25, 2012

MWENDESHA KIPINDI CHA WANAWAKE LIVE JOYCE KIRIA APANDISHWA KIZIMBANI KISUTU LEO ASUBUHI


Pichani ni mwanadada Joyce Kiria anaongoza kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa na stesHeni ya EATV jijini Dra es Salaam, amepandishwa kizimabni leo kwa kosa la kurusha kesi ya mwamama aliye nyang'anywa mtoto na watu wenye asili ya Kihindi wakidai kuwa damu yao haiwezi kulelewa na black people na huku wakiweka madai ya uongo na kusema kuwa mama mtoto huyo ana upungufu wa akili jambo ambalo sio kweli. .

Baada ya kusikiasikia habari hizi nilimuuliza Joyce mwenyewe alienithibitishia kuwa kweli akisema, '' Ni kweli Kesho ntapandishwa kizimbani mahakama ya kisutu kwa kosa la kurusha kipindi cha mama aliyeporwa mtoto wake kwa madai anaugonjwa wa akili..'' baada ya maongezi na Joyce (maana ilibidi nimuulize kama ana hitaji masaada wowote kutoka kwetu maana ni mmoja wa chama chetu cha wamama) Joyce aliendelea na kusema; ''
So mimi naomba wamama wamsapot yule dada kupata mwanae, mimi hata kama watanipeleka jela nitakuwa na amani kama yule mama na mtoto wake wakipata haki yao... Asante sana Tina. Kesi ni kesho asubui(yaani leo ya tz) saa mbili, yangu na ya yule mama pia, pale kisutu''. 


Hayo ndio yalikua maongezi ya Joyce na mimi, sasa tunarudi katika kesi yenyewe, mimi kama mama najua suala zima la uchungu wa mtoto, na wamama wote niliiongea nao wamelaani vikali kitendo hicho, mtu umebeba mimba miezi yote 9 halafu mtu aje kukunyang'anya mwanao kisa rangi...?? hii haiwezekani, tupo Tanzania bado mtu unanyanyaswa kwa rangi ya ngozi yako HII NI HATARI NA JAMBO LISILOKUBALIKA.


( Hongera Joyce na Mungu akutie nguvu uendelee kufichua mambo kama hivi especially kwa wamama wanaoonewa) 

Huyo mama popote alipo akitaka msaada wowote wa kudai mtoto wake awasiliane nasi, tupo wamama wa Kitanzania kwa ajili yake na tutajitahidi kadri ya uwezo wetu kumsaidia.....kama mama ni mzima na anauwezo wa kulea mwanae inakuweje mumnyang'anye kisa mna hela????!!! HAPANA HAPANA haitawezekana, kama mnadai ana matatizo ya akili wakampime kwanza sio kuonea watu bila sababu hapa...na nyie majaji wa hio kesi  Mungu anawaona kama pesa imetembea hapo, hamna hata haya..........mmmxxxhhhhhhhhh 

No comments:

Post a Comment