Na.Ashura
Mohamed-Arumeru
Mbunge wa
Jimbo la Arumeru Mashariki Bw.Joshua Nassari ameipongeza halmashauri ya Meru
kwa kupata hati safi kutokana na ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) baada
ya halmashauri hiyo kuwa na usimamizi mzuri wa fedha za umma.
Akizungumza
katika baraza la madiwani la lililofanyika katika halmashauri hiyo bw.Nassari
alisema kuwa halmashauri nyingi zinashindwa kusimamia matumizi bora ya fedha
halia ambayo inapelekea hamlashauri hizo kupata hatia chafu ama za mashaka.
Bw.Nassari
alieleza kuwa ili kuhakikisha kuwa halmashauri hiyo iweze kuendelea kufanya
vizuri ni wazi kuwa ushirikiano wa karibu wa viongozi hao unahitajika bila
kujali itikadi za vyama vya siasa ili
wananchi wa jimbo hilo waweze kupata maendeleo.
Aidha alisema
kuwa pindi halmashauri inapopata hati chafu serikali kupiti Wizara ya Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) hupunguza fedha za miradi ya maendeleo ama
kutopeleka kabisa kutokana na kuona kuwa kama halmashauri hizo hazina mahitaji
ya fedha kutokana na matumizi mabaya hali ambayo inapelekea miradi ya maendeleo
kurudi nyuma.
Pia alieleza
kuwa swala la fedha ni tatizo katika
halmashauri nyingi hivyo ni vyema kama kuhakikisha kuwa halmashauri inakuwa na
mipango madhubuti na mikakati ili miradi mbalimbali ya maendeleo isirudi nyuma
wala kuyumba.
Lakini hata
hivyo bw.Nassari alieleza wazi kero ya gari la Zimamoto katika halmashauri ya
Meru ni kubwa lakini jitihada za makusudi zinahitajika ili kwa kushirikiana na
halmashauri hiyo ili gari liweze kupatikana ili kupunguza madhara pindi ajali
za moto zinapojitokeza.
No comments:
Post a Comment