Saturday, July 28, 2012

RAJABU MAOJA AMTISHIA MAISHA GOTTLIEB NDOKOSHO WA NAMIBIA

Agombea mkanda wa Afrika wa IBF akipeperusha bendera ya Tanzania nchini Namibia




Mtanzania Rajabu Maoja bondia mzoefu katika ngumi za kulipwa kutoka mkoa wa Tanga atapanda ulingoni Septemba 1 kupimana ubavu na bondia Gottlieb Ndokosho bingwa wa ngumi nchini Namibia.


Mpambano huo unaofanyika katika jiji na Windhoek, nchini Namibia unawakutanisha mabondia wawili ambao wanazimudu vizuri ngumi ulingoni. Hii ni mara ya kwanza kwa bondia wa Kitanzania kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika nje ya nchi tangu mpambano katia ya Iraq Hudu na Ali Said wa Kenya ulivyofanyika jijini Mombasa mwaka 2000.


Wawili hao wataumana kwenye mpambano uliopewa jina la “The Battle for the Kalahari Desert” (Vita ya Jangwa la Kalahari) na waandaaji wa mpambano huo ambao ni Kinda Boxing Promotion chini ya promota Simon Nangolo wa nchi ya Namibia. Namibia iko Kusini Magharibi mwa bara la Afrika ikikingana na Afrika ya Kusini, Botswana na Angola.


Mtanzania Rajabu maoja anatokea katika jiji la tanga na ni mkali aliyejijengea umaarufu mkubwa katika masumbi hapa nchini. Maoja ni kati ya mabondia wachache wenye majina yanayotishia maisha baadhi ya mabondia wenzake katuka bara la Afrika.


Katika uhai wake wa ngumi Maoja amepigana mapambano 31 akishinda 18 na kupoteza kwa kiduchu mapambano 10 ambayo mengi sio yenye hadhi yoyote ya kumharibia historia yake kwemey ngumi na kutoka sare mapmbano matatu (3)


Naye bondia Gottlieb Ndokosho ambaye ni bingwa wa Namibia amepigana pambano 15 na kushinda 11 wakati amepoteza mapambano 3.


Mpambano huo uliopewa jina la The Battle for the Kalahari Desert (Vita ya jangwa la Kalahari) utasimamiwa na Rais wa Shirikiso la ngumi la Kimataifa bara la Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi. Aidha Ngowi ndiye Rais w kamiehsni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) na mkurugenzi wa ngumi wa baraza la Ngumi la Jumuiya ya madola.


Watanzania, tumuezi mwenzetu rajabu maoja anapopeperusha bendera ya Tanzania. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

No comments:

Post a Comment