Friday, July 27, 2012

TAMSHA LA 'CHAGGA DAY CULTURAL FESTIVAL' SASA KUFANYIKA JUMAMOSI LEADERS CLUB


Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul Maganga (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu tamasha maalum la siku ya Wachaga  lililodhaminiwa na Pepsi, litakalofanyika siku ya Jumamosi Julai 28,Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, ambapo pia litasindikizwa na bendi za Msondo Ngoma, Twanga Pepeta na vikundi vingine vya ngoma ya asili, (Kushoto) Ni Fredrick Mtaki, Ofisa Mahusiano wa kampuni hiyo.
********************************************
BENDI  Kongwe na zenye ushindani mkubwa nchi za Twanga Pepeta na Msondo Ngoma zinatarajiwa kupiga shoo ya aina yake kwenye tamasha la siku ya Wachaga, (Chagga Day 2012), Julai 28, viwanja vya Leaders.
 
Akizungumza na waandishi wa habari  mapema leo ukumbi wa Idara ya habari Maelezo, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya MyWay Entertainment, Paul  Maganga, walioandaa tamasha hilo lililoadhaminiwa na kampuni ya SBC Tanzania Limited, kinywaji cha Pepsi, alisema  siku hiyo itakua ya aina yake kwa watu mbalimbali na familia zao watakaojitokeza kufurahia kwa pamoja tamaduni za kabila hilo la Wachaga sambamba na makabila mengine yatakayoshiriki tamasha hilo.
 
“Siku hiyo ni ya pekee, kwa familia kujifunza mambo ya utamaduni  wa kabila hilo la Chaga, na makabila mengine  na burudani kutoka kwa bendi hizo za Twanga na Msondo,  pamoja na vikundi vingine vya ngoma ya asili ” alisema  Maganga
 
Pia alisema kua, kutakua na wazee wa  mila ambo watazungumzia asili la kabila la wachaga huku vyakula na vinywaji vya asili kutoka mkoa wa Kilimanjaro, Kiburu, ndafu, shiro, kitawa, macharari, ngararimo, ng’ande, kisusio, mtori, Kisusio na vingine vingi vitakuwepo siku hiyo.
Aidha, Siboka alisema  baada ya Tamasha la hilo la ‘Chaga day’, litafuatia tamasha lingine litakalofanyika Mkoa wa Kilimanjaro, Desemba 22 ambalo litapambwa na sherehe mbalimbali
 
Aidha, Maganga alisema kua, wataendelea kufanya matamasha haya kwa karibu makabila yote yaliyopo hapa nchini ilikuwezesha jamii kutambua mila zao  sambamba na kudumisha utamaduni wa Mtanzania kwa  kuwakumbusha tamaduni zao hii pia itakua ikijenga na kudumisha mahusiano baina ya  makabila mbalimbali  nchini Tanzania.
 
Pia anasema kua, watazania watakao hudhuria tamasha hilo, watapata kujua chimbuko la kuweko kwa  tamaduni zao  yaani mashujaa wa makabila yao, viongozi na machifu waliotawala jamii zao.
 
Maganga pia aliwataja wadhamini wakuu wa tamasha hilo kua ni pamoja naTBL kupitia bia za Safari na Kilimanjaro,  SBC Tanzania (Pepsi), Dstv,Homeshopping Centre,Canocity,Kishen Enterprises, Zizou Fashion, CXC Africa,Giraffe Hotel,BM barber shop,Mlonge Bi Makai, Chili Chili Restaurant, Auckland Safaris &Tours, Clouds Fm, and Alleys Travel &Tours, Dotnata Decorations.

No comments:

Post a Comment