Wednesday, July 11, 2012

VIONGOZO WA NGUMI WASHIKANA UCHAWI KWA KUHARIBIKA PAMBANBO LA CHEKA NA KASEBA



NADHANI EMANUEL MLUNDWA HUKUUSOMA VYEMA MSIMAMO WA TPBO KUHUSU BONDIA FRANCIS CHEKA . NA USITAFUTE UMAARUFU KWA KUTETEA UJINGA AMBAO WEWE MWENYEWE UMEUTENGENEZA KWA MIAKA MINGI SANA KTK TASNIA YA


NGUMI ZA KULIPWA NCHINI TANZANIA ,NA HAYA NDIYO MATUNDA YAKE NI LAZIMA UYALE HUWEZI KUYAKWEPA KABISA.
KATIKA BLOG YA SUPERDBOXING COACH.http://superdboxingcoach.blogspot.com/
MLUNDWA UMEANDIKA KWAMBA KUMFUNGIA-CHEKA NI UNAFIKI VYOMBO VYOTE VILIJUWA KWAMBA CHEKA HATACHEZA, KWANZA MLUNDWA UJUWE -TPBO HAIKUMFUNGIA CHEKA BALI IMEMUONDOWA KTK ORODHA YA MABONDIA AMBAO ITAFANYA NAO KAZI,HII INA MAANA KWAMBA PROMOTA AMBAYE ANATAKA KUANDAA PAMBANO LINALOMHUSU CHEKA ,ASIJE KUOMBA KIBALI CHA  USIMAMIZI WA TPBO.
ANAWEZA KUJA KWAKO PST ,NA ANAWEZA KWENDA TPBC NA CHOMBO CHOCHOTE LKN ASIJE TPBO.
HII SIYO MARA YA KWANZA KWA TPBO KUTOWA MSIMAMO HUU ,TULIWAHI KUTOWA MSIMAMO KAMA HUU BAADA YA VURUGU ZILIZOTOKEA KTK UKUMBI WA PTA KATIKA PAMBANO LA JAPHET KASEBA VS MADA MAUGO ,KWAMBA TPBO HAITATOWA KIBALI KWA PAMBANO LITAKALOMHUSU JAPHET KASEBA KWA SABABU YA VURUGU ZA MASHABIKI WAKE ,WEWE WAKATI HUO ULIKUWA AUSTRALIA NA VENANCE MPONJI.

PIA TULIWAHI KUMKATAA HALIFA KIPAO KUINGIA KTK MAPAMBANO YANAYOSIMAMIWA NA TPBO KWA KUINGIA ULINGONI NA KUMTUPA FRANCIS CHEKA NJE YA ULINGO NA KUMJERUHI.MPAKA KIPAO ALIPOKUJA OFISI ZA TPBO KUOMBA MAELEWANO NA TUKAYAMALIZA.

NA KAMA UNASEMA VYOMBO VYOTE VYA NGUMI ZA KULIPWA VILIJUWA KWAMBA CHEKA HATACHEZA ,NADHANI TPBC SIYO WAJINGA KUTOWA KIBALI KWA PAMBANO AMBALO WALIJUWA KWAMBA HALIPO . NA KWA NINI CHEKA ALIKWENDA KUPIMA UZITO NA KUVILAZIMISHA VYOMBO VYA HABARI KUWATANGAZIA WATANZANIA MAMBO YA UONGO ? KWAMBA WAJE KWA WINGI UWANJA WA TAIFA KUSHUHUDIA JINSI ANAVYOMCHAKAZA KASEBA ? WEWE NDIYE MNAFIKI KWA LEO HII KUTAMKA KWAMBA KASEBA HANA KIWANGO CHA KUPAMBANA NA CHEKA WAKATI WEWE NDIYE WA KWANZA KUTOWA KIBALI KWA CHEKA NA KASEBA KUPAMBANA NA CHEKA AKIWA NA PAMBANO MOJA TU , NA AKIWA NJE YA ULINGO WA NGUMI KWA KIPINDI CHA MIAKA 12 ,JE LENGO LAKO LILIKUWA LIPI KAMA SIO KUTAKA KASEBA APATE MADHARA ,PALE UWANJA WA TAIFA ,PIA ULIWAHI KUMLETEA FRANCI S CHEKA


BONDIA MWENYE REKODI YA PAMBANO MOJA TU KUTOKA UEZBAKSTAN NA WALICHEZA UBINGWA WA ICB,PALE MKWAKWANI -TANGA.
NA PIA KASEBA NI BINGWA ANAYETAMBULIWA NA PST KTK UZITO WA MIDDLE KWA KUMPIGA MANENO OSWALD PALE TRAVERTAN MAGOMEDI ,NAKUSHANGAA SANA JINSI UNAVYOMDHARAU BINGWA WAKO JAPHET KASEBA -PST. PIA UMESHAPELEKA MABONDIA WA TANZANIA DHAIFU KABISA NCHINI THAILAND KWA AJILI YA KUWATENGENEZEA REKODI MABONDIA WA HUKO ,NA WAPO MABONDIA AMBAO MPKA SASA WAMEATHIRIKA UBONGO ;NA HUWASAIDII KWA LOLOTE -MFANO-TU NI RAYMOND RASTA. WEWE HUJALI KABISA.

MIMI NINALOLIONA HAPA WEWE BINAFSI UNA UGOMVI WA SIRI NA TPBC , NA UMECHANGIA KUHARIBU PAMBANO HILO KWA SABABU AWALI LILIPITIA KWAKO PST KABLA YA CHEKA KUTWAA UBINGWA WA IBF-AFRICA CONTINENTAL .


WEWE NI KIONGOZI MKUBWA KTK JAMII NA USIJARIBU KUNIFANYA NIWAONE WAJINGA HATA WALE WALIOKUCHAGUWA UWE MJUMBE WA NYUMBA KUMI PALE KEKO.

NINAJARIBU KUKUMBUSHA KILA MARA JINSI YA KUSHIRIKANA VYEMA NA VIONGOZI WENZAKO ,NA KAMA UNADAI VYOMBO VYOTE VYA NGUMI VILIJUWA KWAMBA PAMBANO HILO HALITAKUWEPO JE ILIKUWAJE WAAMUZI WA PST WALIFIKA UWANJA WA TAIFA BAADA YA KAIKE KUWAITA KWA HOFU KWAMBA WAAMUZI WA TPBC  WALICHELEWA KUFIKA ,NA ILIKUWAJE KIBALI CHA PAMBANO KILITOLEWA NA TPBC HALAFU DAKIKA ZA MWISHO PST IPELEKE WAAMUZI KWA NINI HAWAKUKATAA ? NA WAKATI PST ILIJUWA PAMBANO HALIPO ?JE NI NJAA AU NINI ? JARIBU KUWA MKWELI ,TUNAKUITA MZEE WA UBAYA KWA MAANA TOFAUTI NA UKIYAFANYA HAYA UNATAKA JINA LAKO LIKUVUNJIE HESHIMA.



USIWE FISI DAIMA KUVIZIA MABAKI YA MIZOGA AMBAYO SIMBA AMEYAWINDA ,AKALA NA AKAYADHARAU KWAMBA HAYAMFAI.

MPE HESHIMA YAKE KASEBA KAMA BONDIA YOYOTE ANAYEPASWA KUHESHIMIWA ,SASA NATAKA KUONA UNA USHUJAA GANI WA KUMCHEZESHA BINGWA WA IBF-AFRICA CONTINENTAL NA HALI YA KUWA HUTAKI USHIRIKIANO NA VIONGOZI WENZAKO.

UBINAFSI HAUFAI DUNIANI KWANI UNAISHI NA WATU WENGI ,BALI HAKUNA ATAKAYEKUSEMA KWA UBINFSI WAK UKIWA KABURINI KWANI HAPO NDIPO MAHALI UTAKAPOISHI PEKE YAKO.
MEANDIKWA NAMI ;-
      YASSIN ABDALLAH
USTAADH
     RAIS-TANZANIA PROFESSIONAL BOXING
  ORGANISATION-TPBO

No comments:

Post a Comment