BAADHI
ya walimu wa shule za msingi mjini Iringa wamekigeuzia kibao Chama cha
Walimu Tanzania (CWT) wakipinga mgomo wake wa walimu ulioanza nchini
kote leo na badala yake wametaka waelezwe kwanza mapato na matumizi ya
michango yao ya kila mwezi kwa chama hicho.
“Tunasikia kuna majengo ya walimu yanajengwa nchi nzima, makatibu wa cwt wananuliwa magari, sasa kuna mpango wa kuanzisha benki, lakini hatupewi taarifa ya mapato na matumizi, na hata magari waliyopewa makatibu hayana msaada kwa walimu ambao ndio wenye mali hata kama wakiumwa,” alisema Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mtwivilla,. Sidified Mapunda.

Alisema
mgomo huo unawapa umaarufu viongozi wa chama hicho na hauna maana
yoyote kwa walimu wa kawaida kwasababu taratibu za kuongeza mishahara ya
walimu hazina tofauti na za watumishi wengine wa umma.
Kwa
upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi y a Wilolesi ambayo pia
walimu wake wote walisusia mgomo hu, George Kameka alisema kabla ya
kumgomea mwajiri wao, wanataka kufahamu tangu kutoka kwa chama chao
hicho cha wafanyakazi tangu walimu nchini kote waanze kukatwa asilimia
mbili kwa ajili ya kukichangia, mapato na matumizi yake yakoje.
Alisema
kuna taarifa zisizo rasmi kwamba CWT iko katika mstari wa mbele kudai
maslai ya walimu ili mishahara yao ikipandishwa na wao wapandishe
michango yao.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chemichemi ambayo ni moja kati ya shule zake chache ambazo walimu wake wamegoma, Demetrius Mgohamwende alisema walimu wote 20 wa shule hiyo wamegoma.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chemichemi ambayo ni moja kati ya shule zake chache ambazo walimu wake wamegoma, Demetrius Mgohamwende alisema walimu wote 20 wa shule hiyo wamegoma.
Inaonekana huyo mwalimu anayeuliza asilimia mbili hatimizi wajibu wake hivyo hawezi kudai haki. Yaani sijui anaishi dunia gani. Amuulize mwakilishi wake wa shule mbona kila kitu kiko wazi kuhusu asilimia mbili wanazokatwa
ReplyDeleteInaonekana huyo mwalimu anayeuliza asilimia mbili hatimizi wajibu wake hivyo hawezi kudai haki. Yaani sijui anaishi dunia gani. Amuulize mwakilishi wake wa shule mbona kila kitu kiko wazi kuhusu asilimia mbili wanazokatwa
ReplyDelete