Orly
Ilemba, akiwa nje ya nyumba aliyokuwa akiishi na marehemu kaka yake,
Patrick Mafisango baada ya mwenye nyumba kutoa nje vyombo vya
ndani kutokana na deni la pango.
Baadhi
ya vyombo vya ndani vya aliyekuwa kiungo mahiri wa Simba, marehemu
Patrick Mafisango vikiwa nje ya nyumba aliyokuwa akiishi katika eneo la
Keko Bora jijini Dar es Salaam, baada ya mwenye nyumba kuvitoa nje
kutokana na deni la pango.
Na Andrew Chale
FAMILIA
ya aliyekuwa kiungo mahiri wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba,
marehemu Patrick Mutesa Mafisango iko katika wakati mgumu baada ya
kutimuliwa katika nyumba waliyokuwa wakiishi, Keko Bora jijini Dar es Salaam.
Familia hiyo, ilitolewa nje vifaa katika nyumba hiyo na mmiliki wake, kutokana na kudaiwa kodi ya pango aliyokuwa akiudai kwa muda mrefu uongozi wa Simba.
Akizungumza
kwa masikitiko makubwa jana, mdogo wa marehemu Mafisango, Orly Ilemba,
alisema, mwenye nyumba huyo, Chingweni Mtoro, aliwafuata asubuhi na
kutaka chumba chake kabla ya kutoa vitu hivyo nje ya chumba na kuweka kufuli jipya.
“Nipo
nje tokea asubuhi, hatujafanya lolote, zaidi nalinda vitu vya marehemu,
viongozi wa Simba kila nikijaribu kuwapigia simu hawapokei mpaka sasa
sina la kufanya,” alisema Ilemba.
Alifafanua kuwa, viongozi hao wa Simba walijua mwisho wa kukaa humo, lakini wameshindwa kushughulikia suala hilo mapema mpaka wanakutwa na aibu hiyo.
“Lakini mwenye nyumba huyu, alisema mkataba huo ulitakiwa kufika mwisho Agosti 8, kama walivyokubaliana na viongozi wa Simba, lakini mpaka jana viongozi hao hawakuweza kumalizana naye ndio maana kaamua kufikia hatua hii,” alisema kwa masikitiko.
Mdogo huyo wa marehemu Mafisango, yupo nchini kwa ajili ya kusubiria rambirambi, ambazo klabu ya Simba iliahidi kuzitoa.
Juhudi
za kuupata uongozi wa klabu ya Simba, kujua wana taarifa na wanachukua
hatua gani, zilishindwa kuzaa matunda kwani wahusika, hawakupatikana.
Mafisango kati ya nyota mahiri waliochangia kwa kiasi kikubwa timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita iliyofikia tamati Mei 6, alifariki dunia Mei 17, 2012 kwa ajali ya gari, eneo la Keko, jijini Dar es Salaam.
Juhudi
za kuupata uongozi wa Simba kuzungumzia hali hiyo ilishindikana baada
ya baada ya simu msemaji wa klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga kutopatikana kwa
siku ya jana.
No comments:
Post a Comment