Thursday, August 16, 2012

KOFFI OLOMIDE KIZIMBANI KWA KUMPIGA PRODUCER WAKE


KINSHASA, DRC
KIONGOZI na mmiliki wa bendi ya Quartier Latin ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Koffi Charles Antoine Mumba Olomide, jana alipandishwa kizimabi juzi jijini Kinshasa, akishitakiwa kwa kupigana mtayarishaji (Producer) wake Diego Lubaki.
Habari kutoka jijini humo zinasema ya kuwa, Olomide, mwanamuziki mashuhuri barani Afrika, ameshitakiwa kwa kumpiga mtayarishaji wake huyo wa siku nyingi, kutokana na madai ya kudaiana pesa kiasi cha dola za Kimarekani 3,680.
Olomide, 56, alikamatwa na kufikishwa kituo kimoja cha polisi, kabla ya kufikishwa mahakani juzi Jumatano, kabla ya kutakiwa kurejeshwa hapo jana Alhamisi ili kutajwa rasmi kwa kesi hiyo.
Taarifa zinapasha kuwa, tangu wakati wa mzozo, kukamatwa, kufikisha kituo cha polisi na hatimaye mahakamani, tukio hilo lilivuta hisia za wengi miongoni mwa mashabiki wa mkali huyo na muziki wa Kikongo kwa ujumla.
Olomide aliyetamba na vibao kadhaa kikiwamo cha Force de Frappe ‘Nguvu ya Kupiga,’ alidokezwa mahakamani hapo na hakimu kuwa, iwapo atapatikana na na hatia katika kesi anayotetewa na mawaikili 10, anaweza kufungwa jela miezi sita.
Koffi Olomide mkali mwenye mafanikio makubwa kwenye tasnia ya muziki DRC, uliompa tuzo kadhaa za Kora, ikiwamo ya mwaka 2002 iliyokuja baada ya ile ya Msanii Bora wa Afrika wa mwaka 1998.
Mafanikio yake katika muziki wa Soukouss, elimu kubwa akiwa na Shahada ya Uchumi na Biashara, ni kati ya vitu vilivyoweka jina lake juu miongoni mwa wasanii barani Afrika – ingawa amekuwa akiishi ya nchi yake miaka mingi sasa.

No comments:

Post a Comment