Wednesday, August 15, 2012

MACHOZI ENTERTAINMENT


Box 3209, Dar es Salaam, Tanzania
KAMATI ya maandalizi ya shindano la Miss Ilala 2012, kesho Alhamis saa 5 asubuhi, itatambulisha mbele ya wanahabari warembo 15, wanaowania umalkia wa taji hilo, linaloshikiliwa na Vodacom Miss Tanzania, Salha Israel.
Warembo hao kutoka vitongoji vya Dar City Center, Tabata na Ukonga wamekuwa katika kambi hiyo kwa wiki mbili sasa na wamekuwa wakiendelea na mazoezi katika Club ya Nyumbani Lounge, iliyopo maeneo ya Namanga, Dar es Salaam sehemu ambayo kesho itatumika katika hafla hiyo fupi ya utambulisho.
Miss Ilala 2008, Slyvia Mashuda ndiye mkufunzi wa warembo hao na ikumbukwe Slyvia alishika nafasi ya pili katika Miss Tanzania mwaka ambao Nasreen Karim alitwaa taji la Miss Tanzania.
Wadhamini waliothibitisha katika mashindano hayo ni pamoja na City Sports Lounge, gazeti la Jambo Leo, Nyumbani Lounge, 100.5 Times FM, Uhuru One na 88.4 Cloud's FM na Redds Premmium Cold. Miss Ilala 2012 Itafanyika Septemba 7, mwaka huu katika sehemu ya nje ya Nyumbani Lounge.
Natanguliza shukrani, wanahabari wenzangu
Gadna G. Habash
Mkurugenzi Machozi Entertainment

No comments:

Post a Comment