Friday, August 31, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA NCHI ZISIZOFUNGAMANA NA UPANDE WOWOTE UNAOMALIZIKA LEO IRAN


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika Mkutano wa Kumi na Sita wa Wakuu wa Nchi za Siasa ya Kutofungamana na Siasa ya Upande wowote  unaomalizika leo  mjini Teheran, nchini Iran. Katika hotuba yake, pamoja na mambo mengine alisisitiza msimamo wa Tanzania kuendelea kupigania haki, kutetea wanyonge, kupinga ubeberu na ukandamizaji  kote duniani, pia aliiasa Jumuiya ya Kimataifa  kutatua migogoro yote kwa njia ya amani. Mkutano huo unamalizika leo na Makamu wa Rais, anatarajia kurejea nchini kesho.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano mkuu wa 16 wa kimataifa wa wakuu wa nchi na serikali usiofungamana na upande wowote Duniani, mkutano huo umeanza leo mjini Teheran Iran.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katika mazungumzo na Mkuu wa Itifaki wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Abad Mobin, wakati Makamu wa Rais alipohudhuria mkutano mkuu wa 16 wa kimataifa wa wakuu wa nchi na serikali usiofungamana na upande wowote Duniani. mkutano huo umefunguliwa leo mjini Teheran Iran.
 


No comments:

Post a Comment