Friday, August 31, 2012

MBUYU TWITE ATUA KUIMARISHA UTANI WA JADI YANGA NA SIMBA


 Beki wa kimataifa wa timu ya Yanga ya Dar es Salaam, Mbuyu Twite, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana wakati alipowasili akitokea Rwanda, tayari kwa kujiunga na timu yake ya Yanga baada ya gumzo la muda mrefu na mvutano wa hapa na pale wa Watani wa Jadi Yanga na Simba, ambao kila mmoja alikuwa kijinadi kuwa amemsajili mchezaji huyo huku mmoja akibaki kuambulia manyoya.

Akizungumza na mtandao huu kuhusu kutua nchini huku akiwa ametinga Jezi no 4, yenye jina la Mwenyekiti wa Simba Ismail Rage, beki huyo amesema kuwa yeye ni mchezaji kama walivyo wengine na anatambua kuwa ametua katika timu yenye upinzani mkubwa na mahasimu wao Simba, hivyo yeye ametua kuendeleza Utaji wa Jadi  baina ya timu hizo, na ndiyo maana ameamua kuvaa jezi yenye jina la Rage, ili kuonyesha maana halisi ya  utani huo pamoja na kutokea mtafaruku wa hapa na pale kati ya vilabu hivyo.

Aidha Twite, amesema kuwa ''Namuheshimu sana Rage, na namuomba aniache nifanye kazi niliyotumwa na Baba yangu kama alivyoniamini na kuniruhusu kuja kuitumikia Yanga na kuwarejeshea Faranga yao Simba'' alisema Twite kwa kiswahili kilichopindapinda.

Twite amewataka mashabiki wa Yanga kumuamini na kupuuza yanayoendelea kuenea juu yake kuwa huenda akikosa kuichezea timu hiyo kutokana na kuchanganya madawa na kusema kuwa yeye ni mchezaji halali wa Yanga timu ambayo imefuata taratibu zote zinazotakiwa.

''Ujue hata mimi nilikuwa na wasiwasi japo nilipokea faranga za Rage, kwani hatukufanya vile imefanya Yanga hadi kufikia jana nilipopokelewa na mashabiki wengi wengi wengi sana wa yanga pale kwa uwanja wa Ndege'' alisema Twite.
Mbuyu Twite, akilakiwa na mashabiki lukuki wa Yanga kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana.

No comments:

Post a Comment