Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais John Dramani Mahama wa Ghana
nyumbani kwake jijini Accra leo Agosti 11, 2012 baada ya kumtembelea na
kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans
Atta Mills aliyezikwa jana.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais John Dramani
Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini Accra leo Agosti 11, 2012 wakati
alipomtembelea kiongozi huyo mpya wa Ghana na kumpa pole ya msiba wa
aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitazama ukulima wa kisasa wa manasi yanayolimwa
kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi katika shmaba la Bomarts Farms Ltd.
katika kijiji cha Dobrokatika eneo la Nsawam nje kidogo ya jiji la Accra
leo Agosti 11, 2012. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa shamba hilo Bw.
Anthony Botchway na mwenye suti ya buluu ni Waziri wa Chakula na Kilimo
Mhe Kwesi Ahwol
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitazama manasi yakitayarishwa kwa ajili ya
kusafirishwa na kuuzwa nje ya nchi katika kiwanda cha Bomarts Farms Ltd.
katika kitongoji cha Dobro nje kidogo ya jiji la Accra leo Agosti 11,
2012
No comments:
Post a Comment