Tuesday, August 28, 2012

SIMBA KUJIPIMA UBAVU NA MAAFANDE WA OLJORO KESHO



KESHO Simba itacheza mechi ya kirafiki na klabu ya soka ya Oljoro JKT katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha. 
Mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya Ligi Kuu ya Tanzania inayotarajiwa kuanza baadaye mwezi ujao.
 
Hii itakuwa mechi ya pili ya kirafiki ya Simba kucheza jijini Arusha baada ya ile ya juzi dhidi ya Mathare United ya Kenya.
 Oljoro JKT imetoka kwenye michuano ya timu za majeshi hapa nchini ambapo ilichukua nafasi ya kwanza pamoja na Ruvu JKT.
 Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic amesema atatoa nafasi kwa wachezaji wengi kwa kadri itakavyowezekana kwenye pambano hilo. 
Viingilio vitakuwa ni Sh 5,000 kwa VIP A, Sh 3,000 kwa VIP B na Sh 2000 kwa VIP C. Kiingilio kwa watoto kitakuwa ni Sh 1000.

No comments:

Post a Comment