Friday, August 31, 2012

SUN CITY MABINGWA SAFARI POOL TEMEKE.


Mkurugenzi wa Klabu ya Kurasin City , Isaac Dirangw (kushoto) akimkabidhi Kikombe  nahodha wa timu ya Sun City, Emmanuel Msengi baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa zilizo malizika mwishoni mwa wiki katika klabu ya Kurasini  City,Mkoa wa kimichezo wa Temeke jijin I Dar es Saalaam.Katikati ni Katibu Mkuu wa chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga.


 
Na Michael Machellah
TIMU ya mchezo wa pool ya Sun City,  ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya pool ya 'Safari Lager National Pool Championship 2012' baada ya kuibamiza Mpo Afrika 13-7 katika mchezo wa fainali wa mashindano hayo ngazi ya mkoa wa yaliyofanyika katika Klabu ya Kurasini City Mbagala.

Sun City kwa kutwaa ubingwa huo walijinyakulia Kombe na fedha taslim Sh.700,000 na pia kuwa wawakilishi wa mkoa huo katika fainali za taifa zitakazofanyika Septemba mkoani Mwanza kwa kushirikisha timu 16 ambazo zitakuwa mabingwa kwenye mikoa yao.
Mpo Afrika ilikamata nafasi ya pili na kuzawa kitita cha shilingi 350,000  na mshindi wa tatu katika mashindano hayo walikuwa ni wenyeji ambao ni Kurasini City ambao walizawadiwa shilingi 200,000 na wane ni BMK ambao walizawadiwa shilingi 100,000.
Timu shiriki zingine ambazo ni Bashnet,MTN,East London na SupesStar zilipewa kifuta jasho cha shilingi 50,000 kila timu kwa kufikia hatua ya robo fainali katika mashindano hayo kwa Mkoa wa kimichezo wa Temeke.
 
Upande wa mchezaji mmoja mmoja “Singles” (wanaume), Jackso Steven kutoka klabu ya Mpo Afrika alitwaa ubingwa kwa kumchapa Hassan Hussein wa MTN 5-1,na kujinyakulia kitita cha shilingi 350,000 ambapo Hassan Hussei alikamata nafasi ya pili na kuzawadiwa shilingi 200,000, wakati Hassan Abubakari kutoka klabu ya MTN alikamata nafasi ya tatu na kuzawadiwa shilingi 150,000.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja “Singles” (wanawake),Beatrice Charles kutoka Klabu ya Mpo Afrika alitwaa Ubingwa kwa kufunga Swaumu Hamisi wa Sun City 5-1, na kuzawadiwa shiloingi 250,000 nafasi ya pili ilichukuliwa na Swaumu Hamisi ambaye alizawadiwa shilingi 150,000 na mshindi wa tatu alikuwa ni Madina Idd  kutoka Klabu ya Kurasini City ambaye alijinyakulia shilingi 100,000
Zawadi kwa washindi wote zilikabidhiwa na Mkurugenzi wa Klabu ya Kurasini City, Isac Dirangw ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kilele cha mashindano hayo katika Mkoa wa kimichezo wa Temeke

No comments:

Post a Comment