Bolt akimaliza kinara mita 200 akifuatiwa na Yohane Blake hayupo pichani na Warren Weir nyuma aliyeshika nafasi ya tatu
Usain Bolt kulia akipongezana na rafiki yake Yohane Blake baada ya kumaliza mbio za mita 200
Usain Bolt kushoto akiwa na mshindi wa pili Yohane Blake
LONDON, England
BINADAMU mwenye rekodi ya kasi duniani,
Usain Bolt ameweka rekodi ya kuwa mkimbiaji wa kwanza kutwaa medali za
dhahabu kwenye mbio za mita 100 na 200 za mashindano ya Olimpiki mara
mbili mfululizo.
Bolt
ameweka rekodi hiyo jana usiku, siku nne baada ya kutetea dhahabu ya
mita 100, ambapo juzi alikimbia kwa sekunde 19.32 kumuwezesha kutetea
dhahabu ya mita 200 akifuatiwa na Wajamaica wenzake Yohan Blake na
Warren Weir.
Blake
alikimbia umbali huo akitumia sekunde 19.44, huku Weir akikimbia kwa
sekunde 19.88, wote wakiwa na miaka 22 mitatu nyuma ya Bolt.
Katika
fainali ya mbio za mita 100 Agosti 5, Bolt aliyeonekana kama kushuka
kiwango, alimfunika Blake kwa sekunde 9.63, aliyemgalagaza mkali huyo
katika mbio za majaribio kupata wawakilishi wa Jamaica mwezi uliopita.
Bolt
sasa ameifikia rekodi ya dunia iliyowekwa na Michael Johnson katika
michezo ya Atlanta nchini Marekani mwaka 1996, ambapo kwa ushindi wake,
nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 amepata heshima kubwa aliyokuwa
akiiwania.
Baada
ya kushinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 200, Bolt kama
kawaida yake alishangilia kwa kufunga mikono kana kwamba anasali,
kusujudu ardhini, kunyoosha kidole mbele na juu na kuonesha ishara ya
kufyatua mshale kutoka kwenye upinde.
“Hiki
ndicho ilikuwa nakitafuta na nimekipata. Najivunia sana hatua hii.
Nilikuwa na msimu mbaya lakini nikaja hapa na kufanya nilichotakiwa
kufanya” alisema akihojiwa na BBC.
“Tumekuwa
tukijitahidi msimu wote, tulipeana moyo na hata kuweka shinikizo ili
tufanikiwe, na sasa tunayo furaha,” alisema akijumuisha Wajamaica
wenzake aliokuwa nao kwenye kambi ya timu ya nchi yao.
No comments:
Post a Comment