Friday, August 24, 2012

Wanahabari 20 Lindi, Mtwara wanolewa matumizi ya Internet.



Waandishi wa habari wa Mikoa ya Lindi na Mtwara wakiwa
kwenye Mafunzo ya matumizi ya Internet kwenye ukumbi wa chuo cha SAUT Mtwara leo.
 Mwandishi wa Blog ya Raha za Pwani Mkoani Lindi, Ahmed Abdullaziz naye akiwa kwenye mafunzo hayo yaliyofanyika leo Mkoani Mtwara.
 Waandishi wengine kutoka vyombo mbalimbali wakiperuzi mitandao wakati wa mafunzo hayo.
Hapa wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.
WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuachana na matumizi pekee ya
internet kuandika habari badala yake  kutafuta habari uhalisia wake.
Hayo yameelezwa na  waandishi wa habari wakati wa mafunzo ya matumizi ya internet
kwa waandishi wa mikoa na wilaya za Lindi na mtwara yaliyoandaliwa na
MISA TAN kwa ufadhili wa mfuko wa vyombo vya habari, Mawasiliano na
Maendeleo Finland yanayoendelea katika ukumbi wa chuo kikuu cha Stella
Maris mkoani Mtwara.
Licha ya kuwepo kwa njia rahisi ya upatikanaji wa habari kupitia
mitandao ya internet hapa nchini waandishi wametakiwa kufuatilia
habari halisia kuepukana na kuwepo na mitandao ya uongo inayopotosha
jamii.
Kwa upande wake mratibu wa mafunzo hayo Andrew Marawiti, kutoka Misa
Tanzania akieleza malengo ya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo  wa
matumizi ya internet katika upatikanaji wa habari mbalimbali na
uhalisia wake ili kuepuka na mitandao inayolenga kupotosha jamii.
Jumla ya  waandishi wa habari 20 kutoka mikoa ya lindi na mtwara
wanapata mafunzo ya matumizi ya internet yanayotolewa  na Taasisi ya
maendeleo ya Habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania(MISA
TANZANIA)chini ya Ufadhili wa Mfuko wa vyombo vya Habari, Mawasiliano
na Maendeleo Nchini  Finland (VIKES FOUNNDATION)
Na Ahmed Abdullaziz-Lindi

No comments:

Post a Comment