Tuesday, August 28, 2012

WAREMBO WA KANDA YA MASHARIKI KUANZA KAMBI LEO


Miss Kanda ya Mashariki 2011, Loveness (katikati) akiwa na washindi wenzake, baada ya kutangazwa washindi katika shindano lao lililofanyika mwaka jana.  Warembo hawa ni miomngoni mwa wanaoingia Kambini leo.
********************************
JUMLA ya warembo 14 wanaotarajia kuwania taji la  Redd's Miss Kanda ya Mashariki 2012, Wanaingia kambini mjini Morogoro jioni ya leo tayari kwa kuanza kambi ya maandalizi ya shindano hilo, linalotarajia kufanyika Septemba 1, mwaka huu, katika Hoteli ya Nashera mjini Morogoro.

Akizungumza na mtandao huu, mratibu wa shindano hilo Alexander Nikitas,  alisema kuwa warembo hao walichelewa kuanza kambi yao kupisha zoezi la kuhesabu Sensa ya watu na Makazi.
Ambapo kila mmoja alipaswa kuhesabiwa akiwa katika Kaya yake kabla ya kuingia kambini, ambapo warembo hao pia walishiriki kuhamasisha zoezi la sensa katika maeneo mbalimbali wanayotoka na wale wa Mkoa wa Morogoro wakihamasisha mjini hapo watu kushiriki kuhesabiwa.

Kanda ya Mashariki inaundwa na mikoa minne katika shindano hilo dogo la Miss Tanzania 2012, ambayo ni mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara na Pwani.

Nikitas, aliwataja washiriki watakao ripoti kambini katika Lodge ya Usambara Safari Resort, iliyopo nane nane mkoani Morogoro kuwa ni Zuhura Gora, Allyce Adam na Shakila Hassan kutoka Mtwara.

Wengine mikoa yao kwenye mabano ni Maria Peter, Irene Mweleko na Rose Lucas (Pwani) Irene Veda, Stella Bartazary na Darina Athumani (Lindi) na kutoka Morogoro ni pamoja na Salvana Kibano, Joyce George, Irene Thomas, Betina Msofe na Nafia waziri.

Taji la Miss Kanda ya Mashariki linashikiliwa na Loveness Flavian, ambaye pia ni Miss Sport Woman wa Miss Tanzania 2011. Warembo hao watakuwa chini ya Mwalimu Asha Salehe Miss Eastern Zone namba tatu, 2011. 

Kwa mujibu wa Nikitas wadhamini wa shindano hilo ni Mbunge wa Kilosa Mustafa Mkulo,Redd's, Dodoma wine, Father Kidevu Blog, Auckland Travel Safairi Tour, Clouds Fm, Usambara Safari Lodge, Chilakale Resort, Endepa Event Planner, Jambo Leo, Kitwe General Traders, mtandao wa Sufianimafoto Blog na Simple Easy Car Rental.

No comments:

Post a Comment