Wednesday, August 1, 2012

Yanga, Push Mobile zamwaga bajaj, pikipiki kwa Yanga


Mwandishi Wetu
 
MABINGWA wa kombe la Kagame, Yanga kwa kushirikiana na kampuni ya Push Media Mobile wamekabidhi zawadi za bajaj na pikipiki kwa mashabiki wa timu hiyo walioshinda katika bahati nasibu inayojulikana kwa Young Africans loyalty SMS campaigns for 2012.
 
Washindi hao ambao walitangazwa rasmi katika mechi ya ya fainali ambayo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC na kutwaa kombe hilo kwa mara ya pili ni Roby Revecatus kutoka Mwanza na Amir Jafari (Tabora) ambao walikabidhiwa pikipiki kila mmoja na Finyasi  Vincent  aliyeshinda bajaj.
 
Mabashabiki hao walikabidhiwa zawadi zao makao makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani na Afisa Habari wa  klabu hiyo Louis Sendeu na meneja wa shindano hilo, Talib Rashid kutoka kampuni ya Push Mobile.
 
Rashid alisema kuwa wamefarijika kukabidhi zaidi hizo ambazo zimekwenda sambamba na shamrashamra na ushindi wa timu hiyo.
 
Alisema kuwa kampuni yao iliendesha shindano hilo kwa lengo la kuwapa ufahamu zaidi mashabiki wa timu hiyo kuhusiana na historia ya Yanga na mambo mengine muhimu ya klabu hiyo.
 
“Baada ya Bajaj na pilipiki, shindano linalokuja litakuwa la kuwania gari, hivyo nawataka kukaa mkao wa kula ili kushiriki katika shindano hilo,” alisema Talib.
 
Naye mshindi wa Bajaj, Finyiasi Vicent aliipongeza Push Mobile na Yanga kuendesha bahati nasibu hiyo ambayo imewafanya wao kusheherekea pamoja na ubingwa wa timu hiyo.
 
“Ni faraja kwetu kwa kukadhiwa zawadi zetu sambamba na ushindi wa kombe la Kagame, mimi na wenzangu tunajiona kuwa wenye bahati kubwa kwa kupata fursa hii,” alisema Vincent.

No comments:

Post a Comment