Sunday, September 30, 2012

AWAMU YA KWANZA YA TANZANIA LIVE MUSIC FESTIVAL YAFANANA


MC wa Tamasha hilo Ben Kinyaiya akiwa jukwaani
AWAMU ya kwanza ya Tamasha la muziki wa dansi lililobatizwa jina la Tanzania Music Festival lililoanza jana katika Viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni limefana baada ya wapenzi wengi wa muziki huo wa kufika kwa wingi kujionea wenyewe burudani hiyo.
Akizungumza na mtandao huu mmoja wa watangazaji wa redio Times ambao ndiyo wadhamini wakuu wa Tamasha hilo, Sinda Madadi ‘Cnda King’ alisema kuwa amefarjika kuona watu kufika kuwaunga mkono katika juhudi zao hizo za kukuza muziki wa dansi.
Cnda King amewaomba wale ambao hawakufika jana wafike leo Jumamosi kwa ili nao wapate burudani hiyo.
“Naomba nitumie nafasi hii kuwaomba wapenzi wote wa muziki huu kufika kwa wingi leo Jumamosi September 29, 2012 kwa sababu ndiyo siku ya mwisho ya kuazimisha Tamasha hili” alisema Cnda King.
Muigizaji Jacqueline Wolper ‘Ilham’ akiwa kwenye pozi na Mzee Kitime
Mtangazaji wa kituo cha Redio One, Salma Dacota mwenye njano akiweka pozi mbele ya kamera huku pembeni akiwa na ‘shostito’ wake
Mtangazaji wa kituo cha Redio One, Salma Dacota mwenye njano akiweka pozi mbele ya kamera huku pembeni akiwa na ‘shostito’ wake
Isha Mashauzi akiwajibika jukwaani
Akienda sambamba na wacheza kiduku wa bendi yake hiyo ya Mashauzi Clasic
Raha ya ngoma lazima uingie ucheze, ndivyo wanavyofanya wapiga magitaa wa bendi ya Mashauzi Clasic
Wanamuziki wa bendi ya Akudo Impact nao wakitoa burudani
Njemba hii ilibambwa ikizungurusha nyonga kwenda sambamba na mirindimo ya taarabu
Wacha weeeeeee! Mzungu naye hakuwa nyuma kuzungurusha nyonga baada ya kupagawa na burudani ya Mashauzi
Salma Docota akijibu mashambulizi kwa mzungu
Mwanamuziki wa bendi ya Fm Academia Pacho Mwamba akiwajibika jukwaani
Mama Rolaa Masai akiwa kwenye pozi na Liva Hassan

No comments:

Post a Comment