Thursday, September 20, 2012

CHAMA CHA MADINI NA NISHATI CHAJIULIZA CHAPATA MAJIBU.


Mwenyekiti  na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Madini na Nishati nchini Joseph Kahama akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua mfululizo wa vipindi vine vya televisheni vitakavyoonyeshwa kuanzia mwishoni mwa mwezi huu kutoa elimu juu ya sekta ya madini nchini.
Baadhi ya wadau wa sekta ya madini nchini na waandishi wa habari wakifuatilia kwa makin vipindi  vya televisheni  vilivyotayarishwa na Chama Cha Madini na Nishati nchini vitakavyoonyeshwa kuanzia mwishoni mwa mwezi huu kutoa elimu juu ya sekta ya madini nchini,  wakati wa uzinduzi wake jijini Dar es Salaaam jana.

KATIKA kile kinachoonekana ni kuguswa na malalamiko na maneno ya wananchi juu ya sekta ya madini nchini Chama Cha Madini na Nishati nchini (TCMC) kimekuja na vipindi vya televisheni ili kutoa elimu juu ya namna sekta hiyo inavyoendeshwa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa vipindi hivyo jijini Dar es Salaam juzi Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa TCME Joseph Kahama amesema wameona kwamba ipo haja yakuongeza uelewa kwa jamii juu ya athari zake kwenye jamii kimazingira na uchumi.
Akifafanua zaidi kuhusu vipindi hivyo kahama alisema kuna maeneo manne hasa ndiyo yatakayo gusiwa zaidi kwenye mfululizo wa vipindi hivyo ambayo ni mguso wa madini tangu hatua za awali, mazingira na athari za uchimbaji, mchango wa uchimbaji madini kwenye jamii na upanuaji na ubadilishanaji wa ufahamu na ujuzi (na upanuzi wa wigo wa ajira).
Sehemu ya awali ya vipindi hivyo ni maelezo juu ya namna uchimbaji mkubwa wa madini unavyoendeshwa kuanzia utafiti wa madini hadi kwenye uchimbaji wake, miundombinu yakukabiliana na mazingira ilivyowekezwa na makampuni yanayochimba madini pamoja kiwango cha wafanyakazi wa kitanzania kwenye sekta hiyo.
Aidha vipindi hivyo vitakua vikieleza pia namna makampuni ya madini yanavyogeuza vijiji kuwa miji kutokana na uwekezaji wa miundombinu mbalimbali ikiwemo huduma za umeme na maji kwenye maeneo ya karibu na migodi hiyo.
Kwenye makala ya mwisho ya vipindi hivyo ambavyo vitaanza kurushwa kwenye vituo mbalimbali vya televisheni mwishoni mwa mwezi huu kitaangazia ukuzaji wa ajira kutokana na uchimbaji wa madini ikiwemo maoni ya wachimbaji wenyewe kwenye migodi husika.
Kahama alisema kwenye sekta hiyo kumekua na Changamoto nyingi yakiwemo maneno mengi ya upotosha juu ya sekta hiyo na ndio maana wamekja na vipindi hivyo kutokana na wananchi mbali na kusikia tu lakini pia watapata kuona kwa picha juu ya hali halisi ilivyo kwenye sekta hiyo.
Changamoto nyingine ni ya hivi karibuni pale waziri wa nishati na Madini alipoamua kuongeza kiwango cha Tozo kwa wenye migodi bila kuwashirikisha.

No comments:

Post a Comment