Friday, September 21, 2012

CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU WANAWAKE TWFA CHATANGAZA KAMATI YA UCHAGUZI



Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) kimetangaza Kamati ya Uchaguzi yenye wajumbe watano kwa ajili ya uchaguzi wake unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.
 
Kaimu Mwenyekiti wa TWFA, Margreth Mtaki amewaambia Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo kuwa kamati hiyo itaongozwa na Ombeni Zavala, na itarajia kutangaza mchakato wa uchaguzi huo Jumatatu (Septemba 24 mwaka huu).
 
Aliwataja wajumbe wengine wa kamati hiyo yenye jukumu la kuendesha uchaguzi wa chama hicho kuwa ni Rachel Masamu, Lloyd Nchunga, Nancy Mabula na Maneno Tamba.
 
Pia aliwataka wadau wa mpira wa miguu wa wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika TWFA mara Kamati ya Uchaguzi itakapoanza mchakato.
 
Wakati huo huo, uchaguzi wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kilimanjaro (KRFA) na Manyara (MARFA) unafanyika kesho (Septemba 22 mwaka huu).

No comments:

Post a Comment