Monday, September 10, 2012

CRDB YASAIDIA MATANKI YA KUHIFADHIA MAJI CHUO CHA UALIMU CHA MAURICE


Meneja wa Benki ya CRDB, tawi la Mbagala, Midlaster Nsanzugwanko (wa pili kushoto) akimkabidhi msaada wa tanki za kuhifadhia maji lenye thamani ya sh milioni 1.7 Mkurugenzi wa Fedha na Uendeshaji wa Chuo cha Ualimu Maurice, Sheddy Maurice kwa ajili ya kukabiliana na matatizo ya maji shuleni hapo. Makabidhiano hayo yalifanyika shuleni hapo Mbande nje kidogo ya jijini la Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Biashara za Kibenki, Georgina Simeo. Katikati ni Mkuu wa Chuo  hicho, Kobero Kandonda.

 Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Maurice, Kobero Kandonda (kulia) akipokea msaada wa matanki 2 ya kuhifadhia maji kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB, tawi la Mbagala, Midlaster Nsanzugwanko. Katikati anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Fedha na Uendeshaji wa Chuo cha Ualimu Maurice, Sheddy Maurice.

No comments:

Post a Comment