Thursday, September 20, 2012

DIAMOND KUPATA WENYE VIPAJI KESHO



Na Elizabeth John
MSANII wa Kimataifa wa Tanzania, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema amedhamiria kutoa ajira kwa vijana wa Kitanzania kupitia muziki wengi wenye vipaji mitaani na kwenye sekta nyingine, wasiojua wafanyeje kufikia ndoto zao, hivyo kuhitaji kushikwa mkono na wengine.
Akizungumza na Habari Mseto, Diamond alisema tatizo kubwa ni jamii kuchukulia masuala ya mitindo na muziki kama uhuni na kuuza sura yaani kupata umaarufu tu kwenye televisheni na vyombo vingine vya habari, akisema kuna haja ya kuifanya jamii kuachana na fikra hizo.
“Mimi nitawalipa wote watakaonekana kwenye video yangu, tutakapofanya usaili kesho wale watakaochanguliwa watalipwa, lakini pia hii inaweza kuwa ni kufunguliwa milango kwenye sekta nyingine.

Najua wapo wanaoweza ‘kufit’ kwenye matangazo ya biashara, pia watapata fursa hiyo,” alisema Diamond.
Kuhusu majaji katika mchujo huo utakaofanyika Nyumbani Lounge kuanzia saa 5 asubuhi, aliwataja kuwa ni Raqey Mohammed wa I-View Studios watakaofanya kazi za matangazo, Ally Rehmtulah ambaye ni Mbunifu na Sammy Cool, mcheza dansi na mwalimu.
Kwa mujibu wa Diamond, jaji mwingine ni Missie Popular ambaye ni mwandishi na mwanamitindo anayejua wapi kwa kuwafikisha watu wengine kama alivyofanikiwa yeye kupitia muziki.

No comments:

Post a Comment