Sunday, September 16, 2012

HADIJA MNOGA AANZA KUMTAMBULISHA MGENI KWA MASHABIKI WA EXTRA BONGO



Khadija Mnoga aka KIMOBITEL akiimba wimbo wake mpya "Mgeni" wakati wa utambulisho wake rasmi baada ya kujiunga na Bendi ya Extra Bongo, wakati wa onyesho maalum la bendi hiyo la utambulisho wa mwanamuziki huyo, ulifanyika ndani ya New White House Kimara Korogwe Dar es salaam.
Kimobitel akiimba na Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki,ndani ya New White house wakati wa utambulisho wake rasmi.
Comredi Ally Choki aka Mzee wa Farasi
Kimobitel akizikonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya Meeda Sinza usiku wa kuamkia leo wakati aliokuwa akitambulishwa rasmi kwa mashabiki wa maeneo ya Sinza na maeneo ya jirani.
Makamanda wa Extra Bongo wakiongozwa na Ally Choki mwenye Tsheti nyeupe mbele, kutoka kushoto ni Banza Stoni, Kimobitel na mwisho kulia ni Rogert Hega aka Katapila wakiimba wimbo mpya wa Hadija Mnoga aka Kimobitel.
Ally Choki Mkurugenzi wa Extra Bongo akiimba kwa furaha wimbo wa "Mgeni" ulotungwa na Khadija Mnoga (Kimobitel).

Mwanamuziki Khadija Mnoga (Kimobitel) wiki iliyopita alitambulishwa rasmi kwa waandishi wa Habari kujiunga na Bendi ya Extra Bongo akitokea bendi ya African Stars (Twanga Pepeta)

No comments:

Post a Comment