Thursday, September 6, 2012

HANS POPE ATOA DOLA 1,000 KUSAIDIA MATIBABU YA MODEST


 Zakaria Hans Pope
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Pope (kushoto) akimkabidhi mchango wa dola 1,000 Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Said Kilumanga kwa ajili ya kusaidia matibabu ya mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa Stars, Alfonce Modest. Modest kwa nyakati tofauti aliwahi kuzichezea timu za Simba, Mtibwa Sugar, Pamba, pamoja na Mlandege ya Zanzibar.

Na Mwandishi Wetu

Mdau wa Soka na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba Zakaria Hanspop amekabidhi Fedha Dola za Marekani Elfu Moja kwa Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Simba na Timu ya Taifa "Taifa Stars" Alfonce Modest ili ziweze kugharimia matibabu ya maradhi ya miguu yanayomkabili mchezaji huyo kwa sasa.
Zakaria Hanspope ametoa Fedha Hizo Baada ya Kuelezewa Tatizo linalomkabili Alfonce Modest na amekabidhi Fedha Hizo Kwa Mratibu wa Matibabu ya Alfonce Modest Saidi Kilumanga ambaye ni Mtangazaji wa Radio Magic Fm na Chanel Ten ambaye amekuwa akilishugulikia swala hilo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo jijini Dar es salaam Zakaria Hans Pop amesema ameguswa na matatizo ya mchezaji huyo na kuona ni muhimu kumsaidia ili aweze kuendelea kupata matibabu
Zakaria Hans pop ametoa Rai kwa Taasisi, Jamii na watu Mmoja moja wenye kujiweza kumsaidia Alfonce Modest ili aweze kupata matibabu ya kina kutokana na maradhi yanayomsumbua.
Taarifa za Kuumwa kwa Alfonce Modest kwa mara ya kwanza zilitangazwa na Kip[indi Cha Michezo Cha Radio Magic Fm ambapo Saidi Kilumanga akiongoza kipindi hicho, aliwaomba mashabiki na wadau wa michezo kwa ujumla kumchangia mchezaji huyo ili aweze kupata matibabu Hatua ambayo imeanza kupata mwitikio.

Alfonce Modest ambaye alikuwa akicheza beki ya kushoto katika klabu ya Simba na Taifa Stars anakabiliwa na maradhi ya Miguu kufa ganzi hali ambayo imemsababishia maumivu makali na kushindwa kutembea kama kawaida. Anayeweza Kumsaidia kwa kutoa msaada wa fedha atume kwa njia ya Simu
0718427426 narudia tena 0718427426.
Alfonce Bado anahitaji Msaada wa Shilingi laki Sita Tu ili kukamilisha mchakato Huo Ikiwa pamoja na Malazi na Usafiri wa Kurudi kwao Morogoro

No comments:

Post a Comment