Wednesday, September 5, 2012

KINGWENDU,RINGO,MTANGA,KITALE WATOKA NA SIMU YA KICHINA


MSANII maarufu wa kazi za sanaa nchini Kitale ameungana na Kampuni ya Bau Entatainment ya jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutoa filamu ijulikanayo kama 'Simu ya Kichina' akizungumza na mwandishi wa habari hizi amesema yupo mbioni kutoa filamu hiyo akishilikiana na baadhi ya wasanii wengine maarufu

Kitale Amesema kuwa filamu hiyo itakuwa gumzo jijini kwa kuwa imerekodiwa kwa ubora wa hali ya juu na kuwashirikisha wasanii waliokomaa kisanii nchini

aliwataja baadhi ya wasanii alioshilikiana nao ni pamoja na Ringo,Kitale mwenyewe,Kingwendu,Mtanga na wengine wengi walioshiriki katika filamu hiyo

aliongeza kwa kusema baadhi ya mafundisho yaliyopo katika filamu hiyo ni Ugumu wa maisha waweza kukupa changamoto ya maisha,ambayo yanaweza kukuletea maendeleo,vilevile ugumu wa maisha waweza sababisha tamaa ambayo yaweza kukupelekea kuwa mwizi katika maisha yako na kukusababishia maisha yako kuwa magumu

filamu hiyo kwa sasa ipo mtaani kwa ajili ya kuwapa wapenzi mbalimbali burudani wakiwa majumbani kwao 'Simu ya Kichina' ni moja ya filamu zenye mafundisho kwa jamii ya kitanzxania hivyo si yakukosa

No comments:

Post a Comment