Tuesday, September 25, 2012

MAONYESHO YA SARAKASI YA TIGO MAMA AFRIKA KUANZA JUMATANO SEPTEMBA 26, 2012


Mtaalamu wa Biashara na Masoko wa Tigo Gaudence Mushi (kulia), ambao ni wadhamini wa Maonyesho ya sarakasi ya Tigo Mama Afrika akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alisema watazamaji wajitokeze kwa wingi ili waweze kupata burudani ya aina yake itakayowaacha katika hali ya furaha. Maonyesho ya mwaka huu hayatakuwa  tu bora bali pia yatakuwa ni maonyesho ambayo yanatukuza na kuunga mkono sanaa na utamaduni wa Tanzania kitu ambacho tunaamini kitawatia moyo watu wengine kufanya hivyo. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Mancom Centre, Constantine Magavilla pamoja na Afisa habari wa Tigo Alice Maro.
 Mkurugenzi wa Mancom Centre, Constantine Magavilla (kati) akiongea mbele ya waandishi wa habari kuzunguzia maonyesho yanayotarajia kuanzia Alhamis tarehe 27 Septemba 2012 mpaka Jumapili Novemba 4, 2012 maonyesho ya sanaa ya sarakasi yatafanyika katika ukumbi wa Mancom Centre New world Cinema Mwenge, Dar es Salaam yakiambatana na programu ya nyimbo za kitamaduni na za kisasa, upindaji wa viungo, michezo ya viinimacho, michezo ya angani, michezo ya piramidi, michezo ya ufito na boriti na mingineyo mengi. 
“Tunapenda kuwashukuru Tigo kwa mchango wao mkubwa na kututia moyo katika maandalizi ya maonyesho haya,” alisema Constantine Magavilla Mkurugenzi wa Mancom Centre. “Tunatumaini kuwa watu hawataondoka hapa wakijisikia tu vizuri bali pia watakuwa wajumbe wazuri kwa watu wengine ili kuwashawishi wengine waje kufurahia maonyesho haya,” alisema.
 Waandishi wa habari wakionyeshwa ukumbi utakaofanyiwa maonyesho hayo. Maonyesho ya sarakasi ya Mama Afrika yalianzishwa mwaka 2003 kama shule ndogo ya sarakasi na  bwana Winston Ruddle aliyekuwa Mkurugenzi na mwaanzilishi . Maonyesho ya sarakasi ya Mama Afrika yamekua na kuwa moja ya maonyesho makubwa yenye gumzo na vipaji vya sarakasi na kutoa fursa ya kutambulisha kikundi maarufu kutoka bara la Afrika, ‘Hakuna Matata Acrobats.
Moja ya michezo ya wanyama Mamba itakayoonyeshwa katika maonyesho hayo. Tiketi zinapatikana sasa na zinaweza kununuliwa katika ukumbi wa Mancom ndani ya Centre New World cinema Mwenge, watazamaji watakuta mpangilio wa viti uliopangwa kutokana na bei za tiketi utakaowaongoza wao kuchagua tiketi ya kununua  na idadi ya tiketi wanazohitaji. Bei ya tiketi inaanzia 10000 na muda wa maonyesho ni saa 9:30 mchana na saa 2:00 kamili usiku, Mara tano kwa wiki.

No comments:

Post a Comment