Monday, September 17, 2012

MATONYA, MR NICE, Z-ANTO, MWANAHAWA WAFUNIKA USIKU WA FLEVA ZA DHAHABU DAR LIVE




Mkali wa Bongo Fleva, Seif Shabani 'Matonya' akipagawisha katika Usiku wa Fleva za Dhahabu ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Lucas Mkenda 'Mr Nice' akifanya makamuzi katika Usiku wa Fleva za Dhahabu uliofanyika Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Ally Mohamed 'Z-Anto' akiwarusha mashabiki waliohudhuria ndani ya Dar Live.
Bi. Mwanahawa Ally wa East African Melody akitumbuiza katika Usiku wa Fleva za Dhahabu uliofanyika Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Kundi la New Zanzibar Stars Modern Taarab likiwapagawisha mashabiki.
Kundi la Ngoma za Asili la Nokalandima likionyesha makali yake.
Mwanasarakasi Lwiti Nzoa akionyesha ufundi.
....akizidi kuonyesha mbwembwe zake.
 
Matonya akiimba wimbo wa Vaileth na shabiki.
Mr Nice akizidi kuwapa raha mashabiki.
Z- Anto na kundi lake wakifanya mambo.
Zahir Hamis wa kundi la New Zanzibar Stars Modern Taarab akiwarusha roho mashabiki.
Msanii wa Kundi la Ngoma za Asili la Nokalandima akipagawisha.

WASANII Lucas Mkenda 'Mr Nice', Seif Shabani 'Matonya', Ally Mohamed 'Z-Anto', Bi. Mwanahawa Ally wa East African Melody, Kundi la Ngoma za Asili la Nakalandima na Kundi la New Zanzibar Stars Modern Taarab usiku wa kuamkia leo wamefunika vilivyo katika Usiku wa Fleva za Dhahabu uliofanyika kwenye ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment