Thursday, September 6, 2012

MICHEZO YAHAMASISHWA KUENDELEZWA KILWA

 Isumaili Ahamd almaarufu kwa jina la Zimbwe akiwa kazini kutoa mafunzo ya mpira wa netiboli kwa wasichana aliowakusanya kwenye kitongoji cha taifa Wilayani kilwa na kuunda timu ijulikanayo timu ya netiboli taifa. Kwasasa ndiyo timu pekee ya mchezo huo wilaya nzima ya kilwa ukiondoa timu za wanafunzi walipo mashuleni.
 Zimbwe akifuata mpira juu kwenye kazi yake hiyo yakujitolea ingawa hana mafunzo ya ukocha amekua kama mdhamini na mkufunzi wa timu hiyo ambayo imewahi hata kuwakilisha Wilaya hiyo na kupata zawadi kwa kushinda kwenye micheo yake. Kati ya michezo minane iliyocheza imeshinda michezo mitano.

No comments:

Post a Comment