Tuesday, September 4, 2012

Mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi unaendelea Mjini Bangkok Thailand


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Richard Muyungi (kushoto), akitoa maelekezo kwa Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Bi. Emelda Teikwa katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi unaondelea mjini Bangkok.  Picha na Evelyn Mkokoi
 *********************************
NA EVELYN MKOKOI, BANGKOK
Rais wa mkutano wa 18 wa Dunia wa mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika mjini Doha mwishoni mwa mwaka huu, amekutana na wenyeviti wa bodi mbalimbali za mabadiliko ya tabianchi katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi unaoendelea mjini Bangkok, akiwa na lengo la kujitambulisha na kusikia mategemeo ya washiriki katika mkutano ujao.

Baadhi ya washiriki waliopata nafasi ya kutoa mategemeo yao leo, ni pamoja na mwenyekiti wa kundi la Africa kutoka nchini Swazland, akizungumza kwa niaba ya Afrika alisema kuwa, anaamini kuwa mazungumzo yote ya majadiliano yanayoendelea hapa Bangkok yatakuwa na mafanikio katika mkutano wa Doha kwani yoote yapo ndani ya uwezo wa washiriki wote, na kundi la nchi zilizoendelea wanatakiwa kutimiza  “commitiment” zao ili kuweza kufikia malengo.

Aliongeza kwa kusema kuwa, anaamini kila upande una jukumu la kuufanya mkutano wa Doha kuwa na mafanikio kwani “wote tunajua na tumeona madhara makubwa na  athari zitokanazo na  mabadiliko ya tabia nchi hivyo basi sote tuna wajibu wa kukabiliana na athari hizo. Alisisitiza”

Aidha, mwakilishi huyo wa Afrika alisema kuwa ni vizuri kikaangaliwa kile kinachotakiwa kufanyika mpaka kufikia mwaka 2015, ikiwa ni pamoja na hatua za kuchukua, na kufikia malengo  ya kupunguza joto la dunia.
 
Kwa upande wake Rais wa mkutano  wa  18 wa Dunia wa  mabadiliko ya tabianchi ambaye pia ni Naimu waziri mkuu w anchi ya Qatar,  amewakaribisha washiriki wote na kusema kuwa yupo tayari kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kufikia malengo katika suala zima la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

No comments:

Post a Comment