Sunday, September 30, 2012

MTANZANIA KUPIGANA URUSI


                    TAARIFA KWA VYMBO VYA  HABARI -MICHEZO.


BONDA WA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI TANZANIA CHUPAKI CHIPINDI KUTOKA IRINGA ,
TAREHE 13-10-2012 ATAPANDA ULINGONI NCHINI URUSI KUZIPIGA NA BONDIA- RODION PASTUKH,WA URUSI KATIKA UZITO WA CRUISERWEIGHT ,PAMBANO LA RAUNDI 12.

TAYARI ORGANAIZESHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA [TPBO],TUMESHAPOKEA BARUA ZA KUMUALIKA BONDIA CHUPAKI CHIPINDI KUTOKA  SHIRIKISHO LA NGUMI LA URUSI [RUSSIA FEDERATION OF PROFESSIONAL BOXING ].


CHUPAKI CHIPINDI ANATARAJIWA KUONDAKA NCHINI TANZANIA TAREHE 04-10-2012 KUELEKEA JIJINI NAIROBI [KENYA] KWENDA KUUNGANA NA WAKALA WAKE NDG THOMAS MUTUA TAYARI KWA SAFARI YA KELEKEA RUSSIA. HAPO TAREHE 07-10-2012

TPBO INAMTAKIA KILA LA HERI BONDIA CHUPAKI CHIPINDI KTK SAFARI YAKE NA AKAJIWAKILISHE VIZURI KWENYE BIASHARA YAKE YA MASUMBWI ILI AWEZE KUPATIWA MAPAMBANO ZAIDI NJE YA TANZANIA.

IMELETWA KWENU NAMI;-

YASSIN ABDALLAH -USTAADH

RAIS -TPBO

No comments:

Post a Comment