Tuesday, September 25, 2012

NIMEZAMA YA BABY MADAHA YAKARIBIA KUIVA



Na Elizabeth John 
"Katika albamu hiyo nyimbo ambazo nimemaliza kuzifanyia video ni chache, ingawa bado naendelea na kazi, ambayo naamini mashabiki wangu wataipenda kulingana na ubunifu nilioufanya humo”
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ anajipanga kuachia albamu yake ya pili aliyoipa jina la ‘Nimezama’.
 
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Baby Madaha alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa albamu hiyo ambayo itakuwa na jumla ya nyimbo nane.
 
Alisema nyimbo ambazo zipo katika albamu hiyo ni mpya na kwamba tayari ameanza kuzifanyia video ili kuwapa raha mashabiki wake.
 
“Katika albamu hiyo nyimbo ambazo nimemaliza kuzifanyia video ni chache bado naendelea na kazi, ambayo naamini mashabiki wangu wataipenda kulingana na kazi nzuri niliyoifanya,” alisema Baby Madaha.
 
Baby Madaha aliwataka mashabiki wake waendelee kumpa sapoti katika kazi zake na kwamba kuna vitu vingi ambavyo amewaandalia wasicheze mbali na yeye.

No comments:

Post a Comment