Saturday, September 8, 2012

RAIS KIKWETE AWASILI KAMPALA KUHUDHURIA MKUTANO WA VIONGOZI WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU, AKUTANA NA RAIS WA KAMPUNI YA TBEA CO LTD YA CHINA, AAGANA NA BALOZI WA JAMHURI YA KOREA


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kuagana na Balozi wa Jamhuri ya Korea Mhe. Young-Hoom Kim aliyemtembelea Ikulu, jijini Dar es salaam jana Septemba 7, 2012 baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi nchini. Kushoto ni mke wa balozi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na  Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika hoteli ya Speke Resort Munyonyo jijini Kampala jana Septemba 7, 2012. Rais Kikwete amewasili nchini Uganda leo  kuhudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za maziwa makuu.
 https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=c5efcfe0c1&view=att&th=139a229689d65b9d&attid=0.3&disp=inline&realattid=f_h6ti9ohv2&safe=1&zw&authuser=0&sadnir=1&saduie=AG9B_P-2CrkZwFZoIv7yIISqZzQc&sadet=1347084239186&sads=h083tXjR2uRqO0XXJqBLY6Tv8i4&sadssc=1
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda baada ya mazungumzo mafupi katika hoteli ya Speke Resort Munyonyo jijini Kampala leo Septemba 7, 2012. Rais Kikwete amewasili nchini Uganda jana kuhudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za maziwa makuu
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Makamu wa Rais wa Kenya Mhe Kalonzo Musyoka aliyemtembelea katika hoteli ya Speke Resort Munyonyo jijini Kampala jana Septemba 7, 2012 ambako wote wamewasili kuhudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za maziwa makuu
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Makamu wa Rais wa Kenya Mhe Kalonzo Musyoka aliyemtembelea katika hoteli ya Speke Resort Munyonyo jijini Kampala jana Septemba 7, 2012 ambako wote wamewasili kuhudhuria mkutano wa siku moja wa viongozi wa nchi za maziwa makuu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Kampuni ya TBEA Co. Ltd ya China aliyefika kumtembelea  Ikulu, jijini Dar es salaam, jana Septemba 7, 2012

No comments:

Post a Comment