Wednesday, September 19, 2012

SERIKALI YA ZANZIBAR WASAIDIA NYUMBA YAKULEA WAATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Viongozi pamoja na Vijana wanaoishi katika Nyumba za kurekebisha Tabia kwa watu waliokuwa wakitumia dawa za kulevya { Sober House } hapo Nyarugusu Wilaya ya Magharibi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Baskeli Kijana Mlemavu Badri Ameir Issa ambayo itamsaidia katika harakati zake za Kimaisha. Msaada huo amekabidhiwa hapo Nyumba ya kurekebishia Tabia iliyopo Nyarugusu Shehia ya Pangawe Wilaya ya Magharibi. Kulia yao ni Mlezi Mkuu wa Nyumba hizo Bibi Fatma Sukwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi  vyakula Mshauri Mkuu wa Nyumba saba za kurekebishia Tabia Unguja na Pemba  Bibi Fatma Sukwa  kwa ajili ya kusaidia Vijana wa nyumba hizo.     Wam,wanzo kulia yao ni mlezi wa Nyumba ya kurekebishia watu waliotumia dawa za kulevya ya  Mtaa wa Nyarugusu Shehia ya Pangawe Bwana Badru Nassor Ali.

No comments:

Post a Comment