Saturday, September 15, 2012

SHIRIKISHO LA NGUMI LA KIMATAIFA IBF LAWAPONGEZA WADAU WA NGUMI AFRIKA



Rais wa IBF Afrika Onesmo Ngowi kulia kiwa na Rais wa IBF Duniani Daryl Peoples wakati wa Mkutano Mkuu wa IBF/USBA uliofanyika nchini Marekani katikati ya mwaka huu.
 Logo ya ushirikiano wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) na Chama cha Ngumi nchini Marekani (USBA)

DAR ES SALAAM, Tanzania

SHIRIKISHO la Ngumi la Kimataifa IBF lenye Makao yake Makuu katika jiji la New Jersey, nchini Marekani kupitia ofisi zake za Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba za Uajemi limetwapongeza wadu wote wa ngumi wanaosaidia kuuendeleza mchezo huo barani Afrika. 

Akizungumza na Habari Mseto, Rais wa IBF Afrika, Mtanzania Onesmo Ngowi, alisema kuwa shirikisho hilo linapenda kuwapongezawadau kadhaa wa ngumi kwa mchango uliotukuka katika kusaiduia harakati za kupanua wigo wa maendeleo ya mchezo huo, wachezaji  mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
 
Ngowi alisema kuwa, nchini Afrika ya Kusini: IBF inapenda kumshukuru Branco Milenkovic, wakati nchini Zambia, wanaopongezwa kwa mchango wao ni Captain John Chewe na Anthony Mwamba. Huko Zimbabwe, Ngowi akamtaja Richard Hondo, wakati nchini Ghana waliopongezwa ni Henry Mann-Spain na  Michael Tetteh.

Huko Nigeria, IBF imevutiwa na kupongeza mchango wa Ken Biddle, wakati nchini Ivory Coast John Ajaba alitajwa na kupongeza, kama ilivyokuwa kwa Richard Nwoba wa Misri, ambapo nchini Oman, IBF haikusita kumpongeza Amin Saad Bait-Mabrook. 


Nchini Tanzania, IBF imewapongeza Gabriel Nderumaki, Lucas Rutahinurwa, Titus Kadjanji, Fidel Haynes, Yassin Abdallah (Ustaadh), Nemes Kavishe, Boniface Wambura, Godfrey Madaraka Nyerere, Shomari Kimbau pamoja na Msajili wa Wizara ya Mambo ya Ndani.

Baraza la Michezo nchini (BMT) nalo limeatajwa, kama ailivyokuwa kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, sanjari na kampuni za BIDCO, Pepsi, pamoja na vyombo vyote vya habari vya magazeti, Radio, Televisheni, Blogs na tovuti (Websites) pamoja na wengine wote ambao wamesaidia kwa njia moja au nyingine. 
Ngowi aliongeza kuwa, IBF inaamini kuwa ushirikiano wa wadau wote, mchezo wa ngumi utapiga hatuia na kuchangia maendeleao ya nyota wa mchezo huo nchini, Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi, hivyo kupanua heshima ya mabondia na viongozi wake duniani kote.

No comments:

Post a Comment