Wednesday, September 26, 2012

TBL YATOA SH. MIL 51 KUSAIDIA UJENZI WA KISIMA MAKANYA,SAME



Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL,Steve Kilindo(kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya thamani ya shilingi milioni 51.6 mkurugenzi wa kampuni ya Dr Gogo Engeneering, Godwin Kallaghe (mwenye kofia) kwa ajili ya shughuli ya uchimbaji wa kisima chenye urefu wa futi 120 katika Kata ya Makanya,
wilayani Same, Kilimanjaro hivi karibuni. Kushoto ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk. Mathayo David.

Wananchi katika Kata ya Makanya, wilayani Same wakishuhudia zoezi la utolewaji wa hundi ya kiasi cha sh. milioni 51.6 kwa ajili ya uchimbaji wa kisima cha maji.Hundi hiyo imetolewa na kampuni ya Bia
Tanzania (TBL).
Wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wa TBL, wakiomba dua katika eneo ambalo kisima chenye urefu wa futi 120 kinachimbwa marabaada ya TBL kutoa kiasi cha sh. mil. 51.6 kwa ajili ya shughuli za uchimbaji huo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi, Dk. Mathayo David akizungumza na wananchi katika eneo la Makanya ambako kisima chenye urefu wa futi 120 kinachochimbwa kwa msaada wa sh. mil. 51.6 na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa ajili a shughuli hiyo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Dr. Gogo Engeneering Company Ltd,Godwin Kallaghe akizungumza na wananchi (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi,Kallaghe amesema kazi ya uchimbaji wakisima hicho utafanyika kwa muda wa wiki tatu hadi kukamilika kwake.

No comments:

Post a Comment