Friday, September 7, 2012

WAISILAMU WAANDAMANA JIJINI DAR. Ni ya kupingwa kukamatwa wanaokataa kuhesabiaa, Polisi waufyata, waamuru kuachiwa wanaoshikiliwa nchi nzima. Wisilamu watangaza ushindi, Wasema Bado Mkuu wa baraza la Mitihani Joyce Ndalichako ajiandae mziki wa maandamano utavamia ofisiyake pamoja na Bakwata nayopia kuvamiwa kwa staili ya maandamano mpaka ifutwe. Muda huu wapo hapa Msikiti Kichangani wanapanga Mkakati wa kuandaa maandamano mengine.


 Waisilamu wakiwa kwenye maandamano kwenye barabara ya bibiti jijini Dar es Salasam leo.


 Baadhi ya watu waliacha kazi kwa muda kushuhudia maandamano hayo ya kundi la waisilamu mbele ya jengo la Wizara ya mambo ya ndani.
 Waisilamu wakisubiri viongozi wao waliokwenda kuzungumza na jeshi la polisi ili kukubaliana na madai yao ya kuachiliwa kwa waisilamu wanaokamatwa kwa kukataa kuandikishwa nchi nzima kauli ambayo imekubaliwa na jeshi hilo.
 Jeshi la polisi wakilinda Jengo la Wizara hiyo wakihofia wasilamu kuvamia.
 Hapa wakiendeleza Takibira.
 Marumbano haya  kukosa wakati wakujipanga kwenye eneo hilo.


 Waliocha kazi zao kushuhudia yanayoendelea.

 Kamanda Kova alifika kutaka kuzungumzanao lakini alishindwa na kwenda kuungana na viongozi wa wizara.
 Ilipofika laasiri pakageuzwa msikiti na kuswaliwa hapo hapo.
 Hapa wakisujudu.

 Wakiomba dua maalum.
 Jopo la masheikh wakitoka wizarani kuja kutoa tamko la jeshi mbele ya waisilamu ambalo walikubaliana na madai ya waisilamu kuchiliwa huru kwa watu wote wanao kamatwa kwa kupinga kuandikishwa sensa.
WALIPORUHUSIWA KUINGIA NDANI KUONGEA NA WAKUU WA JESHI LA POLISI ZAIDI TEMBELEA http://saidpowa.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment