Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoliki, akiwajibika mbele ya 
mashabiki wake, kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja
 vya Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Farid Kubanda a.k.a Ngosha the 
Swagadon, akiwaimbisha mashabiki (hawapo pichani) wake waliokuwa 
wamefurika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa 
Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa filamu Bongo, Vincent Kigos 'Ray',akionesha manjonjo yake 
kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, muda mfupi baada ya 
kukaribishwa kwa ajili ya kuwasalimia baadhi ya mashabiki zao waliokuwa 
wamefurika ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Wasanii wa Filamu Steve Nyerere (kushoto), na Aunt Ezekiel wakishindana 
kuonesha uwezo wa kuzungusha mauno yao katika tamasha la Sererengeti 
Fiesta 2012, lililofanyika kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma. 
Sehemu ya umati uliyofurika viwanjani hapo ukifuatilia kwa makini 
makamuzi ya wasanii hao wa Filamu, kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 
2012, mjini Musoma.
Msanii mwenye umbo kubwa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacob Steven 
'JB', akionesha uwezo wa kunengua kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 
2012 ndani ya uwanja vya Karume mjini Musoma. 






No comments:
Post a Comment